Bei ya Petrol yazidi kupaa.

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (Ewura) imetangaza ongezeko la bei kwa bidhaa za mafuta ya petrol na Diesel.
Kwa mujibu wa Ewura bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa TZS 126/lita sawa na asilimia 5.53 na TZS 166/lita sawa na asilimia 7.66 sawia.
Kwa mujibu wa EWURA kuongezeka kwa bei za mafuta katikasoko la ndani kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuendelea kupanda kwa bei za mafuta hayo kwenye soko la dunia.
“Ifahamike kwamba shehena zote za mafuta ya Petroli na Dizeli (kasoro shehena moja) zilizopokelewa katika bandari ya Dar es Salaam mwezi Juni 2018 zilinunuliwa kwa bei ya mafuta ya soko la dunia ya mwezi Mei 2018 wakati zile zilizopokelewa mwezi Mei 2018 zilinunuliwa kwa bei ya soko la dunia ya mwezi Machi 2018,” Anasema Kaimu Mkurugenzi mkuu wa EWURA ndugu Nzinyangwa Mchany.
Ndugu Mchany ameeleza kuwa ongezeko la bei za mafuta nchini katika mwezi wa Julai 2018 limetokana na ongezeko la bei za mafuta katika soko la dunia kwa miezi miwili mfululizo ya Aprili 2018 na Mei 2018.

Soma taarifa kamili hapa

to_sidebar]

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *