Msimamizi ni nani?

SME-tailorManageBizMsimamizi ni kiongozi wa shughuli yoyote ile. Msimamizi wa biashara ana kazi ya kuhakikisha biashara inafikia malengo yake. Pia anatakiwa kuhakikisha wafanyakazi wanafanya kazi zao kwa ufanisi ili kuchangia ufanikishaji wa malengo yao. Kazi kubwa ya msimazi ni kusimamia shughuli za kila siku za biashara katika kufikia malengo yao.

Msimamizi ni lazima awe na ujuzi/stadi zifuatazo:

 1. Stadi ya usimamizi

 2. Ufundi stadi

 3. Stadi za uhusiano wa binadamu

 4. Stadi za kutafuta na kuendeleza wazo la biashara

 5. Stadi ya utoaji maamuzi sahihi

Kazi za jumla za usimamizi:

 1. Kupanga Mipango- Hili ni lile jukumu alilonalo msimamizi juu ya kupanga mipango na vitendo vitavyohusisha kufikia malengo ya mipango husika. Mipango hiyo ni lazima iwe yenye umoja, mwendelezo, na iweze kubadilika kutokana na rasilimali za biashara.

 1. Kutafuta/Kuajiri wafanyakazi- hili pia ni moja ya jukumu alilonalo msimazi, katika kampuni nyingi msimamizi hushirikiana na viongozi wengine katika kutafuta na kuajirii wafanyakazi. Kwenye makampuni au biashara ndogo, kazi ya uajiri hufanyika na uongozi pekee, wakati kwenye makampuni ya wajasiriamali wa kati kazi hii hufanywa na idara maalum ya rasilimali watu.

 2. Kuongoza, Hiki ni kile kitendo cha kuchochea na kuhamasisha wafanyakazi waweze kufikia malengo husika kwa muda mfupi. Ili msimamizi aweze kuongoza vizuri ni lazima awe na uwezo thabiti wa kuelewa tabia na misimano ya wafanyakazi wake.

 3. Kuwa na udhibiti- ni lazima msimamizi awe na udhibiti mkubwa wa taarifa ili aweze kutambua mapungufu na makosa katika ufanyaji kazi, pia mapungufu katika maelekezo na mipango kwa ujumla.

Mahusiano katika kazi za msimamizi

Kazi zote hapo juu zinategemeana, ni lazima msimamizi awe na ujuzi angalau katika kila kazi ili aweze kusimamia shughuli za biashara kwa umakini na ufanisi.

Majukumu ya msimamizi:

 • Msimamizi ni lazima ajiandae kubadilika kimawazo na kimtazamo kwa haraka kama ambavyo wafanyakazi hufanya.

 • Msimamizi ni lazima awajibike kwa shughuli za biashara kwa kuweka adhabu kwa wafanyakazi wanaoshindwa kutimiza majukumu yao na kutoa motisha kwa wale wanaofanikisha kufikia malengo yakiyowekwa.

Jinsi ya kuwa msimamizi:

 1. Wasimamizi huanza kama wafanyakazi wa kawaida katika biashara ambayo wanaisimamia.

 2. Ni lazima uwe na stadi ya ufundi ambayo ni ya muhimu kwa maendeleo ya biashara husika.

 3. Ni lazima awe na ufundi stadi wa juu kulinganisha na wafanyakazi anaoenda kuwasimamia.

 4. Unaweza kupata nafasi ya usimamizi kwa kuzingatia uzoefu au ukubwa.

 5. Ni lazima pia ue na tabia ya kupenda kazi na kalamu ya uongozi.

 6. Inaweza kua ualisababisha mabadiliko makubwa katika maisha ya kazi ya wafanyakazi

Dondoo za muhimu kwa Wasimamizi:

 1. Kua na mipaka kwenye tabia zako.

 2. Usiwe mtu wa kuokoa jahazi, wafundishe wafanyakazi jinsi ya kuboresha ufanyaji kazi wao ila usiwafanyie.

 3. Tafuta njia mwafaka ya kupima mafanikio ya kazi. Pia uwe na jinsi ya kuwajua watu wako vizuri.

 4. Kuwa na maongezi na watu wote. Ongea na wafanyakazi wote unao wasimamia mara kwa mara.

 5. Kuwa imara. Wakati mwingine wafanyakazi watakupatia majaribu  juu ya sharia na viwango utakavyojiwekea.

 6. Jifunze kutoka kwa wengine. Tafuta mabosi wengine utaoweza jifunza kutokana na busara zao. Tafuta watu ndani na nje ya biashara yako.

Kujiandaa na Kazi:

 1. Epuka uoga wa kushindwa

 2. Kuwa tayari kufanya kazi ya msimamizi

 3. Kuwa mtu wa haki kwa wafanyakazi wako

 4. Elekeza nguvu zote katika kufikia malengo yaliopangwa

 5. ifunze zaidi kuhusu kazi, wakati wa kazi na nje ya eneo la kazi

 6. Endelea kujifunza hata bada ya kupandishwa cheo

 7. Tenga muda kuwajua wafanyakazi wako

 8. Zingatia madili/miiko ya kazi na tenga muda kujadili malengo ya biashara na watu wako

Mamlaka na nguvu za msimamizi:

 1. Ni laziwa awe na nguvu, uwezo na haki ya kufanya baadhi ya vitu

 2. Elezea matarajio yako kwa wafanyakazi

 3. Fanya kazi, wafanyakazi wote wawe kitu kimoja

 4. Kua na hamu ya kusikia mambo yanayohusiana na kazi

 5. Usiharakishe kufanya maamuzi

 6. Build support for change by introducing it gradually.

Sifa za Msimazi mzuri:

a) Mwenye mtazamo chanya sehemu ya kazi
b) Mwaminifu kwenye biashara.
c) Kuwa mtenda haki bila kuwa na upendeleo
d) Mwenye kujiendeleza na kuwa na uwezo mzuri wa kuwasiliana.
e) Mwenye uwezo wa kukasimu kazi.
f) Mwenye kukubali changamoto na kuchangamkia fursa za kufanikisha malengo.

Vitu vya kuangalia wakati wa kusimamia Biashara

USIMAMIZI WA MAHESABU YA BIASHARA
• Je, biashara yako ina mfumo wa mahesabu?
• Mfumo huo ni wa aina gani?
• Je, mfumo huo unafanya kazi vizuri?
• Ni nani anayehusika na usimamizi wa hesabu za kampuni?
• Je, ana ujuzi wa kutosha?

USIMAMIZ WA RASILIMALI WATU
Kuajiri wafanyakazi na kutengeneza malipo yao
Kuajiri wafanyakazi
• Utaajri vipi wafanyakazi?
• Kipi kitatumika kama kigezo cha kuajiri watu?
• Vitu gani vitahitajika wakati wa kuajiri watu?
Kutengeneza malipo ya wafanyakazi
• Je, una wafanyakazi wangapi?
• Je, wafanyakazi hao unawalipa kiasi gani?
• Je, ni kiasi gani hutolewa kama kodi?
• Je, ni kiasi gani hutolewa kama michango ya mifuko ya hifadhi ya kijamii?
Kuhifadhi taarifa za wafanyakazi
• Taarifa za wafanyakazi zitahifadhiwa wapi??
• Ni taarifa gani zitakusanywa?
Kupanga majukumu na wajibu wa wafanyakazi
• Nini ni wajibu na majukumu ya wafanyakazi?
• Ni nani anafuatilia kukamilika kwa majukumu hayo?
• Shughuli hizi zitasimamiwaje?
• Vigezo vipi vitatulika kupima utimilifu wa kazi husika?
Kuzuia Ugomvi
• Je, kuna njia zozote zinazotumiwa kuzuia ugomvi?
• Je, njia hizo ni za uhakika?
• Je, wafanyakazi wanaridhika na njia hizo?

USIMAMIZI WA MASOKO NA MAUZO
• Je, utasimamiaje mauzo na masoko yako?
• Je, ni hatua gani utafuata katika kutengeneza mfumo imara wa kutafuta masoko?
• Je, ni njia gani utazitumia katika kutafuta masoko?
• Je, utapimaje ufanyaji kazi wa nia hizo?

 KUSIMAMIA SHUGHULI/KAZI ZA BIASHARA
• Je, utasimamiaje shughuli za bishara?
• Je, utatumia hatua gani kugawa majukumu kwa wafanyakazi?
• Je, utatumia taarifa za mrejesho wa shughuli?
• Taarifa hizo za mrejesho zitapitiwaje?
• Je, taarifa hizo za mrejesho zitatumika kwa namna gani katika kuongeza ufanisi wa shughuli za kila siku za ofisi?

 

Jinsi ya kupanga malengo kwa wafanyakazi (Mwongozo)

Msimamizi lazima awe na kiu ya mafanikio na aweke melengo ya juu kwa wafanyakazi wake. Malengo ya juu yanaleta changamoto kwa wafanyakazi kujituma na kuweka juhudi ili waweze kuyatimiza. Katika kupanga malengo kwa wafanyakazi, maswali yafuatayo ni ya msingi sana:

HATUA YA 1: Kutengeneza lengo linaloeleweka ambalo biashara inategemea kulifikia baada ya muda fulani
• Je, ni lengo gani unategemea kulitekeleza?

HATUA YA 2: Malengo yote yaliyopangwa lazima yatambuliwe na watekelezaji
Je, ni watu wangapi watahusika kwenye mchakato wa kukamilisha lengo husika?
• Je, wanajua kuhusu lengo hilo?
• Je, umegawa majukumu kwa kila mtu?
• Je, kila mtu anajua kuhusu jukumu lake?

HATUA YA 3: Lazima kuwe na tarehe ya mwisho ya kukamilisha malengo
• Je, ni muda gani utatumika kukamilisha lengo husika?
• Je, wahusika wanajua tarehe ya mwisho ya kukamilisha malengo?
• Je, kuna ongezeko la muda kwa malengo yasiyofikiwa baada ya muda uliopangwa kwisha?

HATUA YA 4: Kuwe na mfumo maalum kwa waajiri ili kupima mafanikio ya malengo
• Je, kuna mfumo wa kupima mafanikio ya malengo ya biashara?
• Je, mafanikio hayo yatapimwaje?
• Je, mfumo huo wa upimaji ni wa uhakika?

HAUTA YA 5: Kuwe na mfumo au namna ya kutoa motisha kwa wafanyakazi
• Je, una mfumo wa utoaji motisha kwa wafanyakazi?
• Je, utawa vipi motisha wafanyakazi?
• Je, vigezo gani vitatumika katika kuwapa motisha wafanyakazi?

Upimaji wa ufanisi wa wafanyakazi

Taarifa kuhusu ushauri wa utaalamu wa kisheria

Ujuzi na utaalam wa kisheria kwa mjasiliamali ni njia mojawapo inayosaidia biashara kujiendesha kwa ufanisi.

Inashauriwa kuwa asasi ya kibiashara ikodishe mtaalamu mahsusi katika masuala ya sheria ili kusaidia biashara yake kujiendesha kwa mujibu wa sheria. Masuala ya kisheria katika uendeshaji wa biashara yanayoweza kushughulikiwa na wataalamu wa sheria ni haya yafuatayo:

 • Kutetea jina la biashara, mawazo, uvumbuzi na usajili wake.
 • Kuandaa, kutathmini na kusimamia mikataba ya biashara.
 • Kuwa katika mstari wa mbele katika mijadala ya mikataba ya kiabiashara. na
 • Kusaidia mchakato wa kupata mali za biashara kwa ujumla.

Taratibu za kupata msaada wa kisheria katika biashara

• Ili kubaini shughuli za kisheria na huduma zitolewazo si budi mjasiliamali akafanya utafiti kujua wanasheria waliopo/na utaalamu wao

Masuala ya kuzingatia ili kubaini wataalamu wa sheria

 1. Lazima awe muhitimu katika taaluma ya sheria na amesajiliwa katika chombo cha wataalaam wa sheria;

 2. Lazima abainishe majukumu atakayotaka kutekeleza; na

 3. Shurti akubaliane na mpango wa malipo ambao hautaharibu fedha za kuendeshea biashara.

 • Si budi kujadili masuala muhimu na gharama zinazohusika

 • Si budi kusaini mkataba baada ya pande zote kuridhika na majadiliano kuhusu masuala na hali ya kazi husika

Kwa nini ni muhimu kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati kufuata Sheria?

Sheria ni mkusanyiko wa amri za kudhibiti mahusiano kati ya watu na makundi ya watu katika jamii. Kwa hiyo, kufuata sheria ni muhimu katika jamii yoyote. Katika biashara, pengine ni muhimu zaidi kuzingatia sheria. Uzingatiaji kama huo unahakikisha kwamba biashara ipo kisheria, na inaingia katika mahusiano yanayotambulika kisheria, yanayotekelezeka na kuendeshwa kulingana na sheria za nchi.

Zifuatazo ni baadhi ya sheria za Tanzania zinazoongoza Wajasiriamali Wadogo na wa Kati:

 1. Sheria ya Makampuni yamwaka 2002

Baada ya kusajili, kampuni inapata uwepo huru wa kisheria unaodhibitiwa na sheria unaolazimisha matakwa kadhaa ambayo si budi yazingatiwe na maofisa pamoja na kampuni. Yafuatayo ni baadhi ya matakwa ya kuzingatiwa na kampuni iliyosajiliwa na maofisa wake:

  1. Kuwasilisha mapato ya kila mwaka yanayohusu maelezo yote muhimu ya kampuni hiyo, ikiwa ni pamoja na maelezo juu ya hisa, uongozi, amana na gharama zingine;

  2. Kuwasilisha mahesabu yaliyokaguliwa;

  3. Kuwasilisha mabadiliko yoyote ya taarifa za kampuni kama vile jina la kampuni, malengo na madhumuni ya kampuni, Bodi ya Wakurugenzi, mtaji wa kampuni, madaraja ya hisa, anwani ya ofisi iliyosajiliwa, uteuzi wa wapokeaji, mameneja, maafisa utawala pamoja na taratibu za kufunga shughuli; na

  4. Malipo ya kodi mbali mbali za serikali kuu na serikali za mitaa.

Kampuni na maafisa wake wasipozingatia matakwa ya sheria na kanuni zilizotajwa hapo juu wataadhibiwa kwa njia ya faini ya fedha na wakati mwingine wanaweza kupata mashitaka ya jinai. Uzingatiaji utaipa kampuni uaminifu, utaipa sifa ya kukopesheka kama hali hiyo itajitokeza na kwa ujumla utaipa kampuni msimamo mzuri katika nyanja za kibiashara na kijamii.

 1. Sheria ya Mikataba

Makampuni yanatakiwa kuzingatia masuala na matakwa ya mikataba iliyofungamana nayo. Endapo matakwa ya kisheria hayatazingatiwa mkataba waweza kuwa batili au kubatilishwa kutegemeana na matokeo ya kisheria mahsusi kwa kosa litakalohusika. Kwa hiyo, ni muhimu kuhakikisha kwamba mikataba ya kisheria inayoingiwa na kampuni inatekelezeka kwa kuzingatia matakwa yote ya kisheria. Kunaweza kuwa na haja ya kupata ushauri wa kisheria kabla ili kuhakikisha kwamba biashara itaendeshwa kulingana na sheria ya mikataba.

 1. Sheria ya kazi

Biashara yo yote inatekelezwa kwa msaada wa watu ambao si wamiliki wa biashara lakini ambao ni wafanyakazi wa kulipwa mishahara kwa huduma zao. Sheri za kazi zinaongoza mahusiano kati ya biashara (kama mwajiri) na wafanyakazi wake (kama waajiriwa). Kampuni pia hutengeneza taratibu za kushughulika na mizozo na usuluhishi wake na masuala ya kustaafu pamoja na mafao ya wafanyakazi. Uhusiano chanya wa kikazi ni suala muhimu katika asasi ya aina yo yote, hii inajumuisha na Wajasiriamali Wadogo na wa Kati.

 1. Sheria ya Leseni

Kufanya biashara kunahusisha uzingatiaji wa sheria. Kutegemea na aina ya biashara, sheria imeweka mahitaji mahsusi chini ya Sheria ya Leseni za Biashara Sura ya 208. Sheria hiyo inazuia kufanya biashara bila leseni ya biashara. Kila lesesni ya biashara inatolewa kwa ajili ya biashara husika na katika eneo husika, labda kama kuna eneo maalumu la biashara ambapo leseni ya biashara tanzu hutolewa au kama hakuna ada ya biashara inayoelezwa kulingana na biashara husika. Mamlaka za leseni zina uwezo wa kufunga maeneo ya biashara zinazoendeshwa bila leseni. Kwa kufanya hivyo, mamlaka yaweza kuomba msaada wa polisi au mamlaka nyingine iliyoinidhinishwa.

 1. Sheria ya Ardhi

Sheria ya Ardhi (inayojulikana kama sheria halisi ya mali) ni moja ya matawi muhimu ya sheria nchini. Sheria kuu ya ardhi nchini Tanzania ni Sheria ya Ardhi Sura 113. Ni sheria ya msingi kuhusiana na masuala ya ardhi licha ya sheia ya ardhi vijijini na inaongoza menejiment ya ardhi pamoja na usuluhishi wa mizozo ya ardhi na masuala yanayohusiana na migogoro ya ardhi. Sheria kuu nyingine ya ardhi ni Sheria ya Ardhi ya Vijiji Sura 114. Sheria hiyo inahusiana na utawala na menejimenti ya ardhi vijijini. Kila biashara ina ardhi na kwa sababu hiyo, kampuni ya biashara lazima imiliki ardhi au mali au ikodishe au ipate sehemu yake kwa mmiliki. Kwa hiyo, biashara yaweza kuwa mmiliki au mpangaji. Sheria ya ardhi inatanabahisha uhusiano huo. Ili kuinua mtaji, shurti biashara iwe na aina fulani ya usalama ili iwe kama dhamana. Rehani ya ardhi ni aina ya kawaida ya usalama. Sheria ya ardhi inaruhusu uanzishwaji, usajili na utekelezaji wa mipango hiyo.

 1. Sheria ya Hakimiliki

Katika Sheria ya Hakimiliki Sura 217 pamoja na usajili wa uvumbuzi kuhusu hakimiliki unatekelezwa na ofisi ya Msajili wa Hakimiliki. Uvumbuzi waweza kuwa suluhisho kwa tatizo mahsusi katika nyanja za teknolojia na unaweza kuhusiana na kitu au mchakato wake. Uvumbuzi unasajilika kama ni mpya na unahusisha hatua ya uvumbuzi na utatumika kiuhalisia. Sheria ya Hakimiliki na Haki za Majirani Sura 218 ni aina nyingine ya sheria inayohusiana na Sheria ya Hakimiliki. Sheria ya Hakimiliki inalinda wabunifu ili ubunifu wao utumike kibiashara. Asasi ya kibiashara yaweza tumia hakimiliki baada ya kukubaliana na mmiliki. Mvumbuzi anaweza kumruhusu mzalishaji kutumia hakimiliki yake na kuweza kuruhusu alama ya haki zake kwa mjasiriamali. Alama za biashara na huduma ni aina zingine zaa hakimiliki. Sheria inawaruhusu wajasiriamali fursa ya kusajili alama za biashara na huduma zao ili kulinda masoko yao na heshima kulingana na thamani ya vitu vyao. Mzalishaji mwenye busara yafaa atumie sheria hii kwa kusajili alama ya biashara za huduma zake. Wakati huo huo, ni muhimu kujizuia kutumia alama za wengine kwa sababu yaweza pelekea migogoro na madai ikiambatana na uwezekano wa madhara makubwa sana.

 1. Sheria ya Bima

Inashauriwa kuwa si budi kuwa na aina fulani ya ulinzi dhidi ya madhara katika biashara. Sheria za bima zinatoa utaratibu wa ulinzi huo kwa kuweka bayana sheria zinazosimamia mikataba ya bima kati ya wakata bima na wenye kupata bima. Bima ya moto, bima ya wizi, bima ya magari na bima ya fidia ya wafanyakazi ni baadhi ya bima zinazoweza kukatwa dhidi ya madhara mahsusi katika biashara.

 1. Sheria ya Mirathi

Sheria ya Mirathi inahusu uhamishaji wa haki na wajibu kwa marehemu kwa warithi wake. Mirathi anaashiria mali isiyohamishika na madeni yanayoachwa na mtu baada ya kifo chake, kama thamani ya mali yake inazidi deni au vinginevyo au ameacha madeni tu bila mali. Mirathi inahusu haki na wajibu tu wa marehemu inapotokea hadi muda wa kifo chake lakini yote yanayotokana na baada ya kufungua mirathi. Mwisho, mirathi inaashiria haki ambayo mrithi anaweza kupata mali ya marehemu, kadri itakavyokuwa. Kwa hiyo sheria imeweka taratibu zinazotoa fursa ya haki ili kushughulikia haki za warithi juu ya mali. Biashara zingine zinakufa na wamiliki wake. Kwa upande mwingine, makampuni huepuka vifo vya wanahisa. Wakati mali za wamiliki na wabia zinarithika, zile za makampuni hazirithiwi, ni mali za hisa tu zaweza kurithiwa.

Mpango Mkakati

Mpango mkakati ni andiko linaloainisha tafsiri, madhumuni ya biashara, mwelekeo na masuala yoyote yanayohusu kutekelezwa katika kuanzisha na kuendesha biashara. Kwa maneno ya kawaida, mpango mkakati huainisha masuala yote yanayoweza kutekelezwa katika biashara na kuyapunguza kwa kuacha mambo ambayo biashara yaweza kutekelezwa kwa ufanisi zaidi na hivyo kutanabaisha kufikia madhumuni ya biashara inayoandaliwa. Mpango mkakati ni muhimu kwa maendeleo ya biashara kama njia ambayo biashara inadhamiriwa kufuata kwa muhula maalumu.

Mambo ya kuzingatia wakati wa kuandaa mpango mkakati wa biashara

Hatua ya 1: Kuamua nafasi ya biashara

Kaika mchakato huu, si budi mjasiria mali akaanzisha nafasi ya biashara katika masuala ya fedha (mtaji), muda, rasilimali watu na rasirimali zingine mahsusi zitakazokuwepo kwa matumizi ya biashara. Mchakato huu ni muhimu sana kwani unasaidia kupata tafsiri sahihi katika mazingira ya biashara, washindani na faida za ushindani wa kibiashara, vipengere ambavyo ni muhimu katika uendeshaji wa biashara.

Hatua ya 2: Kubaini masuala ya muhimu kwa ajili ya biashara

Hii ni hatua nyingine muhimu katika uandaaji wa mpango mkakati katika biashara. Kuanzisha masuala muhimu ya biashara husaidia kuandaa vipambaumbele ambavyo biashara italenga wakati wa kuiendeleza. Katika hili, si budi mjasiria mali akatanabaisha madhumuni au ujumbe mahsusi wa biashara na kupata fursa ya kuelewa ili kuandaa mpango utakaolenga katika masuala muhimu ya biashara.

Hatua ya 3: Weka malengo ya mafanikio

Baada ya kubainisha madhumuni na ujumbe wa biashara, si budi mjasiria mali aweke malengo yanayotarajiwa kupatikana katika biashara kwa kipindi maalumu. Mafanikio yanayotarajiwa ni madhumuni yenye mwelekeo ulio wazi pindi madhumuni yatafikiwa. Hii ni muhimu kwwa sababu itasaidia kupima kiwango cha ufanisi katika madhumuni yanayotarajiwa kutekelezwa katika biashara husika.

Hatua ya 4: Panga majukumu kwa wahusika

Baada ya kuandaa madhumuni na kiwango cha mafanikio, kinachofuata ni kuwapangia majukumu wote watakaohusika katika biashara. Ufanisi wa biashara yo yote unahitaji uwepo wa watu mbali mbali ili kufanikisha malengo yaliyopangwa. Ili kufanikisha hili, si budi mjasiria mali akawapangia majukumu watu wote watakaohusika katika biashara kwani mchakato huu si muhimu tu wa kuwafanya watu wajue majukumu yao bali pia waweza kutumika kuwapima/kuwatathmini wahusika kiwango chao kwa ujumla katika kukamilisha kazi zinazohitajika.

Hatua ya 5: Weka mapitio ya muundo

Mwisho, kunatakiwa kuwe na mchakato wa mapitio ya mara kwa mara ya mpango mkakati. Mchakato wa mapitio unahakikisha kuwa sababu zote za kushindwa au kufanikisha biashara zinaingizwa katika mchakato wa kupanga kuanzisha na kuendesha biashara. Pia maboresho hufanyika katika mpango wote ili kuhakikisha kuwa masuala yote yamezingatiwa ili kufanikisha mchakato wa utekelezaji wa biashara.

Masuala yafuatayo ni ya kuzingatia

 • Si budi kila mtu anayefikiria kuwa na biashara au kuendesha biashara awe na mpango mkakati ili kuhakikisha mafanikio na ufaulu katika biashara anayotarajia kuanzisha na kuendesha.

 • Mwingine anaweza kushangaa kwa nini anahitaji mpango mkakati wa kuanzisha na kuendesha biashara wakati ambapo amefanikiwa kibiashara. Ieleweke kwamba kufaulu katika biashara hakuhakikishi uhai wa biashara kwa hapo baadaye. Kwa hiyo, kuwa na mpango mkakati wa kuanzisha na kuendesha biashara kuna hakikisha usalama, ukuaji wa biashara na maisha marefu ya biashara yako.

Angalizo: Tafadhali angalia kiambatanisho kinachoonesha mfano wa mpango mkakati wa kuanzisha na kuendesha biashara.

Orodha ya asasi kwa msaada wa kisheria

Zifuatazo ni faida za Mpango Mkakati wa Biashara:

 • Unatoa fursa ya kuendesha biashara vyema na kuanzisha mwelekeo unaotarajiwa katika biashara;

 • Unawezesha tathmini ya kila mara ya malengo ya biashara;

 • Unasaidia kutoa maamuzi ya busara katika biashara kwa vile kuwa na uwazi wa dira ya biashara kutawezesha kubaini maamuzi mazuri dhidi ya maamuzi mabaya kulingana na malengo ya biashara;

 • Huanzisha biashara endelevu kwa vile kuwa na mpango mkakati kutawezesha kutabiri na kukabiliana na hali mbali mbali za biashara na masoko, hali ambayo inahakikisha maisha ya biashara; na

 • Husaidia kuboresha uendeshaji wa biashara.

Usindikaji wa chakula

USINDIKAJI WA CHAKULA

Kama msindikaji wa chakula, usalama wa chakula ni lazima uwe kipaumbile chako namba moja

Usindikaji wa chakula ni kile kitendo cha kubadili bidhaa ghafi za kilimo kiumbo na kikemikali na kuwa chakula tayari. Katika utayarishaji, usindikaji wa chakula unahusisha kuchanganya viungo ghafi vya chakula ili kuweza kupata chakula ambacho kiko tayari kutumiwa na wahitaji. Kama ilivyo katika nchi nyingine, wajasiriamali ndani ya Tanzania wanaweza kujihusisha na biashara ya kusindika chakula.

Soma zaidi….

Zijue sifa za Mjasiriamali

20151201_133632

Kwa kiasi kikubwa ni vigumu kutaja sifa amabazo lazima mtu awe nazo ili awe mjasiriamali. Ila kuna sifa za jumla ambazo wajasiriamali wengi huwa nazo.

Kabla hatujajifunza sifa za mjasiriamali tuangalie kwanza maana ya Ujasiliamali

Read More….

Kusimamia biashara

Biashara

Mmiliki yeyote yule wa biashara anatakiwa ajue namna ya kusimamia mzunguko mzima wa fedha katika biashara yake

Usimamizi wa biashara unahusu shughuli zote zinazoendana na uendeshaji wa kampuni au biashara, kama vile, udhibiti, uongozi, ufuatiliaji na upangiliaji wa kazi mbalimbali za kampuni au biashara ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Ifuatayo ni baadhi ya miongozo ya usimamizi wa biashara inayoweza kuwasaidia wajasiriamali kuendesha shughuli zao:

 

Soma zaidi….

Baadhi ya sababu zinazofanya biashara kufa

moto

Ni muhimu kwa kila mjasiriamali kuzingatia changamoto zinazoweza kuletwa na eneo atakaloamua kuanzisha biashara yake

Japokuwa biashara nyingi zinazoanzishwa zimekuwa zikifanikiwa, zipo nyingine nyingi ambazo hushindwa kabisa kuendelea na pengine hufa.

Kuna sababu mbalimbali ambazo kwa kiasi kikubwa huchangia kufa kwa baadhi ya biashara. Makala hii inakuletea sababu hizo na inapendekeza mbinu za jinsi ya kukabiliana na kushindwa huko

Soma zaidi….