Hii ni ile hali ya kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara wenye biashara au maeneo ya biashara yanayofanana kwa ajili ya kuuuziana bidhaa, kununua biadhaa au kufanya biashara kwa kushirikiana. Hii husaidia kukutanisha wajasiriamali wa aina zote kutoka nchi zinazoendelea na zilizokwisha endelea kibiashara kwa lengo la kuongeza masoko, ujuzi, mitaji na teknolojia.

ZIFUATAZO NI BAADHI YA TAASISI VINAZOSAIDIA KUKUTANISHA WAFANYABIASHARA

1. Maendeleo ya Ushirikiano wa Kibiashara wa Ubalozi wa Uholanzi

  1. Aina hii ya ukutanishaji wa kibiashara hufanywa na ubalozi wa Uholanzi nchini Tanzania. Wajasiriamali wa kitanzania wanashauriwa kuomba kuunganishwa kibiashara na wafanyabiashara wa kiholanzi kupitia ubalozi wao nchini. Ushirikiano huu lengo lake kuu ni kuanzisha mfumo wa muda mrefu wa ushirikiano wa kibiashara kati ya wajasiriamali kutoka nchi zinazoendelea na Uholanzi. Ushirikiano huu wa kibiashara unatazamiwa kupelekea fursa ya uchumi wa kusafirisha bidhaa nje ya nchi au kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi, na sehemu ya mchakato huu inahusisha kampuni au mjasiriamali wa kitanzania kutembelea kampuni mbali mbali za kiholanzi ili kupata mshirika wa kibiashara watakaoendana kisekta.

Nani anaweza Kushiriki?

Ushirikiano huu wa kibiashara ni kwa ajili ya wajasiriamali wa aina zote kutoka Tanzania ambao wanafanya shughuli zao kwa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa, wanaotafuta mshirika wa kibiashara.

Kwa maelezo zaidi kuhusiana na kipengele hiki tuma barua pepe kwenda mmf@rvo.nl

Jinsi ya kuomba

Mchakato wa kutafuta mshirika wa kibiashara kutoka ubalozi wa Uholanzi unafanywa kwa kujaza fomu zinazopatikana ubalozini.

Unatakiwa kujaza taarifa mbali mbali muhimu kama vile maelezo sahihi ya kwako binafsi na kampuni yako kwa ujumla, huduma/bidha ambazo kampuni au biashara yako inashughulika nazo, na maslahi/fursa gani unadhani huduma au bidhaa zako zitachangia kwa mfanyabishara unaemtafuta kutoka uholanzi.

Baada ya kujaza fomu yako itume kupitia mmf@rvo.nl

 

Kukagua Maombi yako

Baada ya kurudisha fomu ya maombi Ubalozi wa Uholanzi kwa kushirikiana na wataalamu waliopo watapitia maombi yako kuangalia kama yanaridhisha. Kama matokeo ya maombi yako ya kutafuka mshirika yataoneka kuwa na matokeo chanya ubalozi utaanza kumsaidia mjasiriamali kupata mshirika kutoka washirika waliopo kutoka Uholanzi.

Baada ya kupitisha na uhakiki wa maombi yako kwa niaba ya mfumo huu wa kutafuta mshirika, atachaguliwa mtaalamu kutoka uholanzi wa sekta unayotaka kuifanyia bishara ka ajili ya kukupatia mshirika husika kutoka Uholanzi ambaye mtashirikiana katika biashara zenu.
Baada ya kupatikana mshirika mwenye sifa uanzotafuta, mjasiriamali anaweza kukaribishwa kwenda Uhoolanzi kukutana na mshirika husika, ingawa hapa mjasiriamali atatakiwa kujigharamia usafiri na malazi, Mpango wa ushirika utagharamia malipo ya mtaalamu atakayehusika kuwakutanisha na kumsaidia mjasiriamali katika makubaliano.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Ubalozi kupitia
Anuani
Umoja House, Ghorofa ya 4
Garden Avenue
Dar es Salaam
Simu: +255 22 219 40 00
Nukushi: +255 22 211 00 44

2.Mradi wa Ushirikiano kati ya Sekta za Umma na sekta Binafsi Wa Ubalozi wa Ujerumani

Mradi huu unaendeshwa na kusimamiwa na serikali ya Ujerumani kwa kushirkiana na mashirika mbali mbali kupitia ubalozi wake uliopo nchini Tanzania.
Mradi huu unawaunganisha wajasiriamali wa kitanzania waliorasimisha biashara zao na wafanyabiashara wa kijerumani kwenye sekta zitakazoshabihiana kimaslahi na kibiashara.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mradi huu wasiliana na wawakilishi wa ubalozi wa Ujerumani wanaohusika na kitengo hiki kupitia anuani zifuatazo

Umoja House
Mtaa wa Mirambo /Garden Ave., Ghorofa ya 2
SLP 95 41
Dar-es-Salaam
Tanzania
Simu: (+255) 22-211 74 09-15
Nukushi: (+255) 22 211 29 44
Barua pepe: info@daressalam.diplo.de
Tovuti: www.daressalam.diplo.de

3. Mpango wa Uendelezaji wa Sekta Binafsi wa Mfuko wa Msaada wa Denmark

Ushirika wa kibiashara wa Danida unatoa msaada kwa shughuli za kibiashra zinazoonesha dalili ya kuwa na maslahi kwa washirika wake kutoka Tanzania na Denmark. Wazo la mradi linaweza tolewa na mjasiriamali kutoka aidha Tanzania ambaye atakuwa anatafuta mshirika katika sekta anayojihusisha nayo au mjasiriamali kutoka Denmark ambaye ameona fursa ya kibiashara kwenye ukanda wa Afrika mashariki au Tanzania.
Kwa kawaida hakuna sekta maalum inayopatiwa au kuwezeshwa kwenye ushirika huu, ila msaada wa kukutanishwa unatolewa kwa zile shughuli za kijasiriamali ambazo zinaonekana kuwa na matokeo chanya kwenye maendeleo.

Mawazo ya mradi yatayokuwa yanalenga muingiliano wa kibiashara kwa ukanda wa Afrika Mashariki yatakuwa katika nafasi nzuri ya kusaidiwa.
Programu hii kutoka Ubalozi wa Denmark inamuwezesha mjasiriamali kupata ruzuku kwa mambo yafuatayo:

  • Kutambua kusaidia kupata mshirika kwa aijili ya biashara au kampuni
    Safari za mafunzo mbali mbali ya kijasiriamali
  • Msaada wa upembuzi wa maandalizi ya kuingia ubia na kujifunza
  • Kujaribu mpango wa biashara kama utakuwa unaweza kufanyika na kuleta faida
  • Kubadilishana uwezo wa kiutendaji
  • Msaada wa kiufundi, mafunzo na msaada wa kiusimamizi katika biashara
  • Kuwezesha biashara ya usafirishaji bidhaa au huduma nje ya nchi
  • Kuboresha mazingira ya kufanyia kazi

Kwa maelezo na msaada zaidi tafadhali wasiliana na:
Albert Nkinda
Mratibu wa Programu ya Ushirika wa Kibiashara wa Danida
SLP 9171
Dar es salaam, Tanzania
Simu: +255 (22) 216520
albnki@um.dk

Masaa ya kazi Jumatatu- Alhamisi saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni
Ijumaa sa mbili asubuhi mpaka saa saba mchana