Mtaji

Bank+of+Bongo

Kwa kawaida, biashara nyingi huanzishwa kwa kiasi kidogo cha mtaji

Ili kuanzisha biashara wahitaji fedha ya kuanzishia pamoja na fedha ya kuendeshea biashara yako walau itayotosha mwaka wa kwanza au hata miezi sita ya kwanza.

Biashara nyingi zaweza kuanzishwa kwa kutumia mtaji mdogo. Baadaye, kadri biashara inavyokua na kupata uzoefu, faida itakayo patikana kutokana na biashara hiyo yaweza kutumika katika kukuza biashara. Ili kupunguza matumizi wakati unaanzisha biashara yako inashauriwa kutoajiri watu au kuajiri wachache sana. Kazi nyingine waweza anza kwa kuzitekeleza mwenyewe. Kufanya kazi nyingi mwenyewe ni njia nzuri ya kujifunza kuhusu biashara yako na inakufanya uwe na uwezo mkubwa wa kugawa majukumu kwa wengine hapo baadaye.

Unapofikiria kuhusu mtaji zingatia masuala yafuatayo:

Gharama za kuanzishia: Hizi ni gharama ambazo hujitokeza kabla ya kuanza kupanga matumizi ya mwezi wa kwanza. Gharama hizi, ni zile gharama za jumla zitakazo hitajika ili uweze kuanzisha biashara. Kwa mfano, kampuni nyingi mpya hugharimia shughuli za kisheria, ubunifu wa alama, vipeperushi, uchaguzi wa eneo, maboresho na gharama nyingine ndogo ndogo.

Gharama za wafanyakazi: Hii ni mahsusi kwa biashara zinatohitaji kuajiri wafanyakazi. Katika hili, mtu anahitaji kupanga idadi na viwango vya mishahara itakayolipwa kwa wafanyakazi watakaoajiriwa.

Leseni na Usajili: Kama inavyoelezwa katika sehemu ya leseni na usajili (www.brela.go.tz), kuna gharama kadhaa ambazo zinahitajika zilipwe na kila mtu anayetaka kuanzisha biashara ili kuiwezesha biashara iwepo na kutambulika kisheria. Gharama hizo lazima zitathiminiwe katika mtaji wa kuanzishia biashara.

Kwa taarifa zaidi kuhusu usajili na leseni za biashara, bonyeza hapa

Mali/Mtaji wa kuanzishia: Mali halisi za kuanzishia huhusisha samani pamoja na vifaa vitakavyo hitajika mwanzoni wakati wa kuanzisha baishara yako. Vitu hivi ni lazima viwekwe kwenye gharama za jumla za kuanzisha biashara. Mfano wa mali hizo ni vifaa, samani za ofisi, mashine/mitambo, na kadhalika.

 

Mfano wa Jedwali la gharama za kuanzisha biashara kulingana na Mtaji wako