Ewura yasitisha kupitia maombi ya leseni ya IPTL

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imefuta mkutano wake na wadau wa sekta ya nishati wa kujadili kuhusu  maombi   ya kampuni   ya   uzalishaji   umeme   ya INDEPENDENT  POWER  TANZANIA  LIMITED (IPTL) kuomba  kuongezewa  muda  wa  leseni yake  ya  kuzalisha  umeme.

IPTL iliomba kuongezewa  muda  wa  leseni yake  ya  kuzalisha  umeme  kwa  kipindi  cha  miezi  55  kutokea  tarehe  15 Julai  2017.

Mara tu baada ya Ewura kutangaza nia hiyo ya IPTL kuomba kuongezwa mda wa kuzalisha umeme wananchi na wasomi mbalimbali walijitokeza kupinga vikali hatua hiyo.

Hata hivyo EWURA inasema kuwa iliwasiliana  na  Wizara  ya  Nishati  na  Madini  ili  kupata  maoni  yake  kwa  mujibu  wa kifungu  cha  7  (3)  cha  Sheria  ya  EWURA,  Sura  ya  414  ya  Sheria  za  Tanzania.

Wizara  ya  Nishati  na  Madini imetoa  mapendekezo  ya  kuwapo  na  mashauriano  zaidi  kati  ya  Wizara,  EWURA  na  wadau  mbalimbali  wa sekta ndogo ya umeme kabla ya kuendelea na mchakato wa maombi ya Mwombaji. Kutokana  na  maoni  hayo,  EWURA  inasitisha  mchakato  wa  kushughulikia  maombi  ya  leseni  ya  Mwombaji ikiwa  ni  pamoja  na  upokeaji  wa  maoni/mapingamizi  dhidi  ya  maombi  hayo  mpaka  hapo  yatakapotolewa maelekezo mengine

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *