Faida za Kuridhisha Wateja

Wateja wanaporidhika inakuwa rahisi hata kulipa bei ya juu zaidi na hivyo kuleta faida zaidi.

Wateja walioridhika husambaza sifa nzuri za biashara na hivyo kuleta wateja wapya.

Wateja wa zamani hurudi tena

Kuongezeka kwa wateja huongeza mauzo na faida pia.

Wateja wakiridhika huongeza hata ari ya mfanya biashara na wafanyakazi, na hivyo kuboresha zaidi utendaji kazi wao.

Namna Ya Kufanya Mara Mteja Anapofika Kwenye Biashara Yako

Msikilize vizuri ili ujue mahitaji yake. Kama hujaelewa, uliza.

Onyesha ukarimu na mhudumie mteja kwa tabasamu.

Mhudumie mteja kwa makini.

Kubali malalamiko na ujibu kwa uangalifu

Zungumza kidogo, Sikiliza zaidi.

Kila mara jaribu kuwa na subira, kwa sababu wateja wengine ni wazito kuamua.

Mambo Ya Ziada Ya Kumtendea Mteja

Ubadilishe salamu/kufuatana na vile mteja aelekeavyo.

Kuwa na tabia sahihi/adilifu.

Kujiamini.

Fikiria kwa makini.

Onyesha hisia kuwa unapenda kumsaidia mteja.

Jaribu kugundua mambo anayopendelea mteja hata bila yeye kuyasema.

Weka mazingira yatakayojenga uhusiano na mteja hata kwa baadaye.

Kushughulikia Malalamiko Ya Wateja

Hakikisha umefahamu vizuri malalamiko yaliyoletwa kwako.

Omba radhi hata kama makosa ni ya mwenzio.

Kama mteja ana malalamiko mengi, shughulikia moja moja huku ukimhakikishia kwamba malalamiko yake yote yatashughulikiwa.

Kama unadhani uwezo wako wa kutatua tatizo la mteja umefika mwisho, usiendelee kumchelewesha bure, mhusishe mtu mwingine ambaye unadhani ataweza kuleta utatuzi.

Wafuatilie wateja wako ili uone kama wameridhika kwa kuongea nao, kuwapigia simu au kwa mawasiliano mengine yoyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *