Taasisi zinazotoa huduma za kifedha

Kuna taasisi nyingi sana zinazotoa huduma za kifedha Tanzania, zifuatazo ni baadhi ya taasisi hizo

VISION FUND TANZANIA

Taasisi hii inafuata maadili ya Kikristu kwa kusaidia watu wenye mahitaji mbalimbali. Taasisi imejikita katika kusaidia watu ambao hawapati misaada mbali mbali inayohitajika kutoka kwa taasisi au vyama vyenye majukumu hayo.
Kwa sasa, Vision Fund ni taasisi ndogo ya kifedha inayokua kwa haraka kwa kutumia mapato yanayopatikana kutoka katika vyanzo mbalimbali. Taasisi huwekeza kwa kusaidia jamii wanayohudumia kwa njia ya mikopo na kadhalika.

Aina ya huduma zitolewazo
1. Huduma za Kibenki
i. Akaunti Binafsi
ii. Akaunti ya Biashara
iii. Akaunti ya Ushirika

2. Mafunzo kwa Wateja
Mafunzo hutolewa kwa kushirikiana na taasisi zingine zisizo za kifedha katika jumuiya kupitia mipango maalum. Mafunzo yanajumuisha maarifa ya kifedha na ya kimaisha, kuendeleza biashara na kupata masoko na kadhalika.

3. Mikopo
• Mikopo ya Vikundi vya Biashara
Taasisi huto mikopo maalum kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wadogo walio katika vikundi vya kibiashara. Mikopo hiyo inawapa fursa wajasiriamali wasiokuwa na nafasi kutoka kwenye taasisi nyingine kuu za mapato. Wajasiriamali wote wa mjini na vijijini wana nafasi ya kupata mikopo. Wajasiriamali ambao wanastahili kupewa mikopo ni wale ambao wanafanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa kwa ajili ya usimamizi wa shughuli za kibiashara.

• Mikopo ya Mshikamano ya Kujiendeleza
Walengwa ni vikundi vidogo vidogo vya wajasirimali wa biashara ndogo zenye mitaji mikubwa kiasi kwa kuanzia shilingi milioni mbili (2,000,000/). Mikopo ni maalum kwa ajili ya wajasiriamali wa maeneo ya mijini, wakopaji waliovuka kutoka mikopo ya kibiashara (wajasiriamali waliokwisha rejesha mikopo yao kupitia mikopo ya vikundi vya kibiashara) na watu wengine wanaweza kupata mikopo hii.

• Mikopo Binafsi
Hiyo ni mikopo kwa ajili ya mjasiriamali mmoja moja ambao wamekwishavuka ngazi za mikopo iliyoainishwa hapo awali na hata wakopaji wapya wanaweza kupatiwa mikopo hii maalum kwa ajili ya watu wa kati kati ya miji. Wajasiriamali hao ni wale ambao walikwisha kopa na kurejesha mikopo ya vikundi vya biashara na mikopo ya mshikamano ya kujiendeleza.

• Mikopo ya Kilimo
Mikopo ya kilimo hutolewa kwa wateja ambao wanamiliki biashara zenye mtiririko mdogo wa kifedha. Wateja ambao husubiri kwa miezi michache ili kupata mapato ya biashara zao wanaweza kupata mikopo hii. Mikopo hii ni kwa ajili ya wakulima katika maeneo ya vijijini hasa maeneo ambayo shirika la World Vision Tanzania linafanya kazi.

Kwa maelezo zaidi soma hapa

TWIGA BANCORP

Twiga Bancorp inatoa huduma zifuatazo:

1. Huduma
• Bima za tuzo (Premium)
Twiga Bancorp inatoa mikopo ya kulipia bima kwa mkupuo kwa wateja wa bima katika kampuni zao. Wateja wa bima watalipa deni la bima kwa kila mwezi kwa kipindi cha kuanzia miezi mitatu (3) hadi miezi kumi (10), kutegemea na makubaliano yatakayofikiwa kati ya mteja wa bima, kampuni inayotoa huduma za bima na Benki ya Twiga Bancorp. Hii inategemea na kiasi cha bima ambacho biashara au mali imewekewa na muda ambao mjasiriamali atatakiwa kurudisha kiasi alichodhaminiwa kwenye bima.

• Mikopo ya Makadirio ya Rasimu ya Biashara (Overdraft)
Mikopo ya muda mfupi ambayo haizidi miezi kumi na mbili (12). Mikopo inatolewa kulingana na makadirio ya kibiashara yanayotokana na uhalisia wa namna biashara inavyokwenda ikiambatanishwa katika maombi ya mkopo. Twiga Bancorp hurekebisha muda wa mikopo kulingana na tathmini itakayofanyika. Kiwango cha hakitazidi asilimia 75 ya kiwango cha mtaji unaohitajika. Mjasiriamali yeyote ambaye amerasimisha biashara yake anaweza kupatiwa aina hii ya mikopo.

• Mikopo ya Muda Mfupi
Mikopo ya muda ni mikopo ya kifedha kwa ajili ya kuwezesha kupata vifaa, bidhaa za mitaji au kitu chochote kulingana na aina ya mradi uliokusudiwa na mjasiriamali. Kabla ya kupatiwa mkopo, mkopaji atatakiwa kuwasilisha ripoti ya upembuzi wa mradi ambayo itapitiwa na kuthaminishwa uwezekano wake kiufundi na kifedha. Twiga Bancorp hurekebisha muda wa mkopo kulingana na tathmini itakayofanyika. Kiwango cha mkopo hakitazidi asilimia 75 ya kiwango cha mtaji unaohitajika. Wajasiriamali wote ambao wanafanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria wanaweza kupata aina hii ya mkopo kwa kwenda katika tawi lililo karibu la Twiga Bancorp ili kupewa taarifa kamili kuhusu mikopo hii.

• Mikopo ya Kufungashia Bidhaa
Hii ni mikopo maalum kwa ajili ya kuwawezesha wajasriamali wanaosafirisha bidhaa nje ya nchi. Mkopaji atapewa mkopo baada ya kuwasilisha orodha ya mahitaji aliyopokea kutoka kwa mteja. Mikopo hii ni kwa ajili tu ya wajasiriamali ambao wanasafirisha bidhaa au huduma za ujasiriamali wao nje ya mipaka ya Tanzania. Mjasiriamali anayesafirisha biashara yake nje ya nchi atahitajika kutoa vithibitisho kuhusu bidhaa anazosafirisha na benki itajiridhisha kama anafaa au hafai kupewa mkopo wa namna hii.

• Barua za Mkopo
Hizi ni nyaraka ambazo hutolewa kwa wafanyabiashara wa Tanzania wanaoingiza bidhaa kutoka nje ya nchi ili kuwezesha shughuli zao za kibiashara kupitia benki au taasisi za kifedha za kigeni. Barua hizi za dhamana ya mkopo hutolewa ili kuthibitisha shughuli na uwezo wa mjasiriamali katika biashara husika.

• Mkopo wa Kulipia Bili za Kibiashara
Twiga Bancorp inaweza pia kufadhili aina mbalimbali za shughuli za biashara na biashara kupitia mapunguzo ya gharama au majadiliano ya nyaraka za biashara au bili mbali mbali za biashara. Mjasiriamali wa Mtanzania ambaye shughuli zake anaziendesha kwa mujibu wa sheria anaweza kupata mkopo huu kwa kwenda katika benki husika na kupewa taratibu za mkopo.

• Mkopo wa kukodi/kununua Vitendea kazi
Mkopo unahusisha mjasiriamali kuwezeshwa sehemu ya fedha ya kununua magari kwa ajili ya kufanyia biashara na pia kwa ajili ya kununulia vifaa vya ujenzi na vifaa vingine vya kibiashara visivyozidi thamani ya shilingi milioni 500. Mikopo hii ni kwa ajili ya wajasiriamali wa kati na wakubwa ambao shughuli zao zinaendeshwa kwa mujibu wa kanuni na taratibu za biashara nchini Tanzania. Aidha, mfanyabiashara awe katika sekta ya ujenzi, kilimo na shughuli nyingine yoyote ambayo inahitaji vitendea kazi.

• Mikopo kwa Ajili ya Mali isiyohamishika/Nyumba
Benki ya Twiga Bancorp inafikiria kutoa mikopo ili kusaidia wakopaji kukidhi gharama za ujenzi wa nyumba zao au majengo mengine. Hii inamaanisha kuwawezesha kununua malighafi kwa ajili ya ujenzi, kulipa wajenzi na gharama nyingine zinazohusiana na ujenzi. Mikopo hii ni kwa ajili ya wajasiriamali wote Watanzania. Maelezo zaidi juu ya mikopo hii kwa mjasiriamali ni kuwa anashauriwa kwenda katika tawi la Twiga Bancorp lilo karibu na yeye.

• Mikopo kwa ajili ya Waajiriwa
Mikopo ya benki ya Twiga pia inawajumuisha watu walio na ajira za kudumu au kimkataba na walio na haki ya kupata mafao. Waajiriwa wana nafasi nzuri ya kupata mikopo wakiwa wanaungwa mkono na waajiri wao kuhusu suala zima la namna ya kurudisha mikopo wanayodhamiria kuchukua. Mikopo hii ni mizuri kwa wafanyabiashara tofauti kama vile kampuni binafsi na za umma, wizara/idara za serikali, vyuo vya mafunzo, mashirika yasiyo ya kiserikali, bunge, kampuni za biashara na aina nyingine za biashara zinazoajiri watu mbali mbali.

2. Akaunti Binafsi
• Akaunti ya Akiba ya Twiga
• Akaunti ya Watoto ya Twiga
• Akaunti ya Sherehe/Likizo ya Twiga

3. Akaunti ya Haraka ya Twiga
Akaunti hii imebuniwa maalum kwa ajili ya wafanyabiashara ili kuwawezesha kukamilisha mahitaji ya biashara zao ya kila siku. Akaunti hii inaweza kufunguliwa na mtu mmoja mmoja, makampuni na taasisi.

Kwa maelezo zaidi soma hapa

BENKI YA JUMUIYA YA MUFINDI (MuCoBa)

Benki hii inatoa huduma na bidhaa mbalimbali kwa ajili ya wajasiriamali kama ifuatavyo:
1. Mikopo
MuCoBa inatoa aina nne tofauti za mikopo kwa masharti kwamba mjasiriamali anayehitaji kukopa ni lazima awe amefungua akaunti katika benki hii kwa kipindi kisichopungua angalau miezi mitatu kabla ya kuomba mkopo.

• Mikopo ya Waajiriwa
Mikopo hii hutolewa kuunga mkono shughuli za kiuchumi zenye faida ndani ya wilaya ya Mufindi. Vfuatavyo ni vigezo vikuu kwa mikopo:
– Uwepo wa biashara na mkopaji ni lazima kwake kuw na uzoefu wa angalau mwaka mmoja katika biashara anayoiombea mkopo;
– Dhamana ni kigezo kingine cha msingi ambapo dhamana zinazokubalika zinajumuisha nyumba, ardhi na viwanja vilivyoendelezwa, magari, mashine, na amana ya fedha iliyohifadhiwa katika Benki ya Mufindi na dhamana inathaminishwa kwa kiwango cha mkopo ulioombwa; na
– Mkopo ni wa kipindi cha miezi 18 na muda wa ziada kabla ya kuanza kurejesha mkopo kwa mtu mmoja mmoja ni mwezi mmoja. Ingawa muda wa ziada kabla ya kuanza kulipa deni umewekwa kulingana na aina ya biashara, kwa mfano, kwa wanaoshughulika na kilimo na shughuli zinazotegemea aina ya mazao yanayolimwa.

• Mkopo wa Kikundi
Hii ni mikopo inayotolewa kwa mtu mmoja mmoja ndani ya kikundi ili kuunga mkono shughuli zao ndogo ndogo za uchumi. Mikopo hii ni maalum kwa ajili ya wafanyabiashara ambao hawakidhi masharti ya mikopo kwa benki nyingi kutokana na ukosefu wa dhamana stahiki na wanahitaji kiasi kidogo cha mikopo.
Katika aina hii ya mkopo, wateja ni lazima wajichague na kutengeneza vikundi vidogo vidogo vya watu kati ya watano na saba na kuunda vikundi vya watu kati ya 20 na 40.

MuCoBa inatoa mikopo kwa kikundi ili kurahisisha usimamiaji katika kulipa mikopo husika. Kwa kutumia aina hii ya mikopo, inasadia kuwapunguzia gharama za usafiri wateja wanaoishi maeneo ya nje ya mji hadi umbali wa kilometa 100 kutokea Mafinga. Mwanakikundi anapata mkopo kulingana na kiasi wanakikundi walichoweka katika akaunti zao kwa wastani wa 1:3 (weka 1 kopa 3). Kwenye akiba, mikopo inadhaminiwa kutokana na msukumo wa kurudisha mikopo baina ya wanakikundi wenyewe. Si budi kikundi kipokee mafunzo kuhusiana na namna ya kuweka akiba kabla hakijapewa mikopo.

Muda wa aina hii ya mkopo ni miezi 12 na kipindi au muda utakaopewa kabla ya kuanza kulipa mkopo utanpangwa kulingana na aina ya biashara mtu anayofanya ingawa mara nyingi huwa ni kwa mwezi mmoja.

• Mikopo ya Ushirika
Hii ni mikopo inayotolewa kwa ajili ya vikundi vya kuweka akiba na kukopa (SACCOS) ili kuviwezesha kuwakopesha wanachama wao. Lengo ni kuviongezea uwezo vikundi hivyo ili viweze kufikia mahitaji ya wanachama wao. MuCoBa inatanua huduma na utendaji wake kwa sababu inavitumia vyama vya ushirika kama wateja wao wakuu. Mikopo kwa vyama vya ushirika hulipwa ndani ya mwaka mmoja lakini chini ya mazingira ya dharura inaweza kuwa hadi miezi 18.

BENKI YA JUMUIYA YA MWANGA (Mwanga Community Bank Limited, MCBL)

Huduma Zitolewazo:
1. Mikopo
• Mikopo ya Biashara
Hii ni kwa ajili ya wafanyabiashara kupata mitaji wa kufanyia biashara zao. Aina hii ya mikopo hutoa mkopo wa haraka na wa uhakika kwa ajili ya mahitaji ya kibiashara ya muda mfupi au muda wa kati. Mfanyabiashara anayestahili kupata mkopo ni yule ambaye ana akaunti ya kuhifadhia fedha katika benki ya Mwanga na biashara yake ni lazima iwe imerasimishwa.

• Mikopo ya Vikundi vya Mshikamano
Mikopo ya vikundi vya mshikamano inawalenga watu wa kawaida ambao vipato vyao vinategemea biashara au shughuli zao binafsi za kiuchumi, ambao wanapungukiwa na taarifa rasmi za kifedha na mahitaji mengine ya kumbukumbu za kiakaunti na ambao wanakosa dhamana halisi. Mikopo hii inakusudiwa kwa wajasiriamali wadogo kabisa wenye nafasi ya kuboresha viwango vya maisha na biashara zao.

Mahitaji ili kuweza kupata mkopo huu:
• Akiba ya Lazima
• Kikundi cha watu watatu hadi watano
• Rehani ya mali binafsi
• Rehani ifanywe na wanakituo cha shughuli za biashara
• Rehani ifanywe na wanakikundi wakuu
• Lazima wawe na biashara zinazoendelea kufanyika

• Mikopo ya Wekeza
Hii ni mikopo ya jumla kwa ajili ya vikundi kama Benki za Jumuiya za Vijiji (VICOBA) ili kuwakopesha wanachama wao. Mkopo lazima ulipwe ndani ya kipindi cha uendeshaji wa shughuli husika.
Mahitaji ili kuweza kupata mkopo huu:
• Kuweka akiba kwenye Benki ya Mwanga
• Taarifa za vikao zilizowekwa sahihi na angalau asilimia 51 ya wanachama wote wa kikundi
• Nakala ya katiba ya chama na cheti cha usajili kutoka kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya
• Fomu ya maombi iliyojazwa

• Mkopo wa Kilimo
Ni mkopo maalum kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali wanaojishughulisha na kilimo, usindikaji, masoko, shughuli za uzalishaji kupitia wanyama kama ufugaji kuku, ng’ombe na nguruwe, uvuvi, ufugaji samaki, ufugaji nyuki na usindikaji wa vyakula. Kipindi cha mikopo na kurejesha mikopo hutegemea aina ya shughuli husika iliyoombewa mkopo.
Mahitaji ili kuweza kupata mkopo huu:
• Shughuli inayofanyika ni lazima iwe na faida
• Kuwa na akaunti ya akiba katika benki husika
• Fomu ya maombi ya mkopo wa kilimo iliyojazwa
• Mradi unaoombewa mkopo ni lazima uwe katik sekta ya kilimo

• Mikopo ya Muda Mfupi (Overdraft)
Mikopo ya muda mfupi kwa ajili ya kutatua matatizo na mahitaji ya kila siku ya wateja wa benki

• Mikopo ya Gesi ya Mimea
Mikopo hii ni maalum kwa ajili ya wateja wanaohitaji kujenga vyanzo vya gesi ya mimea katika majumba yao kwa matumizi ya umeme na kupikia.
Mahitaji ya Mikopo:
• Mkopaji ni lazima awe na akaunti katika benki ya MCBL
• Awe na shughuli inayomuingizia kipato
• Fomu ya maombi ya mkopo iliyojazwa

2. Huduma za Kibenki
a. Akaunti ya Akiba
• Akaunti ya Akiba ya Kawaida
Hii ni akaunti ya riba yenye kiwango fulani cha kufungulia akaunti kama kitakavooneshwa na benki. Kiwango cha kufungulia akaunti kitakuwa kikibadilika kulingana na muda na maamuzi ya benki kama itakavyooneshwa kwenye kitabu cha mwongozo wa benki.

• Akaunti ya Akiba ya Wekeza
Hii ni maalum kwa ajili ya vyama vya kuweka na kukopa vya vijijini. Akaunti hii haitozwi makato ya mwezi huku ikiwa inapata faida/riba ya asilimia 3 kwa mwaka. Kiwango cha chini cha kufungulia akaunti ni shilingi 20,000/ za Kitanzania.

• Akaunti ya Akiba ya Faidika
Hii ni akaunti ya akiba yenye riba ambapo mteja anatakiwa kuweka kiasi cha shilingi 500,000/. Kutoa pesa kwa matumizi mbalimbali inaruhusiwa lakini kiasi kinachobaki hakitakiwi kupungua shilingi 500,000. Kiasi cha riba kinaanzia asilimia 6 hadi asilimia 8. Wasiliana na Benki kwa maelezo zaidi.

b. Akaunti ya Sasa (Current Account)
Hii ni akaunti ya hundi ambayo huweza kufunguliwa na mwenye akaunti ana uwezoo wa kuchukua fedha kwa wakati wowote kama fehda taslimu au kwa hundi. Ili kuendesha akaunti, mwenye akaunti atapewa kitabu cha hundi. Akaunti hizi zimegawanyka kama ifuatavyo:
• Akaunti ya sasa ya mtu mmoja mmoja – hii inamilikiwa na mtu mmoja na inahitaji shilingi 50,000 kufungua
• Akaunti ya sasa ya Kampuni/Taasisi – hii ni maalum kwa ajili ya makampuni au taasisi zilizosajiliwa kisheria na kianzio kwenye akaunti ni shilingi 100,000.

c. Akaunti ya Uwekezaji (Fixed Deposit Account)
• Akaunti ya Uwekezaji ya Muda
Hii ni akaunti ya uwekezaji ya muda ambayo inamwezesha mwekezaji kupata riba kulingana na kipindi atakachochagua kwa kuanzia siku 35 hadi miezi 12. Akaunti hii ya uwekezaji ina fursa ya uamuzi kwa muda wa uwekezaji wa fedha za mteja.

• Akaunti ya Uwekezaji ya Hekima
Hii ni akaunti ya uwekezaji kutegemea na makubaliano maalum. Ni akaunti ambayo humwezesha mteja kupata riba katika msingi wa miezi katika kipindi cha kuanzia miaka miwili hadi miaka mitano. Kiasi cha riba kinategemea hazina ya dhamana ikijumlisha asilimia kati ya 0.5 hadi asilimia 1.

Kwa taarifa zaidi soma hapa

BENKI YA WANAWAKE TANZANIA

HUDUMA ZITOLEWAZO MIKOPO

• Mikopo ya Biashara
Hii ni maalum kwa ajili ya kuwaunga mkono wajasiriamali kwenye biashara zao nchini Tanzania. Mkopo huu unawapa wajasiriamali mtaji wa kufanyia biashara na kuwekeza ili kuwasaidia kutimiza malengo yao.
Mahitaji ya Mkopo
• Akaunti zilizofanyiwa ukaguzi kwa muda wa miaka mitatu
• Cheti cha ulipaji kodi
• Maamuzi ya kupitisha mkopo kutoka Bodi ya Benki ya Wanawake Tanzania
• Mpango wa Biashara/Pendekezo la Biashara
• Cheti cha namba ya utambulisho wa mlipa kodi
• Muda wa mkopo ni miezi sita hadi thelathini na sita (miaka mitatu)
• Cheti cha usajili

• Mikopo ya vyama vya Ushirika
Mahitaji ya Mkopo
• -Barua ya utambulisho
• -Cheti cha usajili
• -Barua ya dhamana
• -Dondoo za kikao cha mwisho
• -Katiba
• -Majina na mawasiliano ya waomba mikopo
• -Vitambulisho vya watia sahihi walioidhinishwa
• -Picha za paspoti za maofisa
• -Kuweka katika benki asilimia 25 ya mkopo walioomba

HUDUMA ZA KIBENKI
a). Akaunti Binafsi
• Akaunti ya kibiashara
Akaunti hii ni maalum kwa ajili ya changamoto za kila siku za kibiashara. Ni suluhisho madhubuti la kuwasaidia wajasiriamali kufikia kwa haraka malengo yao ya kibiashara.
Faida za Akaunti ya Biashara
• -Inakuhakikishia usalama wa biashara kwa sasa na baadaye
• -Inatoa viwango vya riba vyenye manufaa na baada ya muda mteja ataweza kufurahia viwango vya kuvutia vya riba kutoka kwenye akaunti yake.
• -Ni rahisi kufungua na mteja anaweza kufungua akaunti kwa kiasi cha kuanzia shilingi 3000/= pekee. Pia humchukulia mteja kulingana na mazingira na muda wowote ana uhuru wa kuangalia akaunti yake.
b) Akaunti ya Vyama vya Ushirika ya Tajirika
Aina ya akaunti hii ni maalum kwa ajili ya kuunga mkono vyama vya ndani vya ushirka vya kukopa na kuweka akiba, taasisi ndogo ndogo za kifedha au kikundi cha watu ambacho kimetengeneza umoja wa kuweka akiba na kukopeshana fedha. Akaunti hii ni ya ujumla kwa ajili ya kuunga mkono taasisi au wateja lengwa. Lengo la akaunti hii ni kuhudumia vyama na taasisi za kifedha zilizojikita katika kusaidia jamii kama vile vyama vya ushirika vilivyosajiliwa na vyama vya kuweka na kukopa.
Faida za Akaunti hii
• -Kufungua akaunti kwa haraka
• -Hakuna urasimu katika ufuatiliaji
• -Viwango vya riba ni vya kiushindani na kuvutia
• -Vitabu vya kutolea fedha
• -Mafunzo ya kujenga uwezo kwa viongozi wa vyama vya ushirika
• -Maelezo ya hali ya akaunti yanatolewa bure kwa kila baada ya miezi mitatu kama yatahitajika
• -Uwezo wa kubadilika na kupata taarifa za akaunti ya mteja kwa wakati wowote atakaohitaji
• -Ulipaji wa mikopo unaobadilika kulingana na mazingira na hali ya biashara
• -Haki ya kupata mikopo ni kulingana na akiba
• -Kulipa washirika wa biashara kwa kutumia hundi zao za mezani
c) Akaunti ya Muda Mfupi ya Uwekezaji (Call Account)
Akaunti hii imebuniwa kwa ajili ya kuunga mkono wafanya biashara wakubwa. Ni akaunti inayotoa riba bila kuwa na muda maalum wa kuweka fedha na mwekaji fedha anaweza kuchukua fedha zake kwa muda wowote. Hii ni akaunti kwa ajili ya uwekezaji wa muda mfupi kwa wateja wanotaka kupata faida kwa kuweka kiasi kikubwa cha fedha. Faida yake inapatikana pindi tu mwekaji anapoamua kutoa fedha zake.
Faida za akaunti hii:
• -Kuna riba ya hadi asilimia 2 kwa mwezi
• -Masharti yasiyobadilika
• Kiwango cha chini cha kuweka ni shilingi milioni 200

Kwa maelezo zaidi soma hapa

BENKI YA JUMUIYA YA MERU

Huduma za Kibenki
• Akaunti ya Akiba
Hii ni akaunti kwa ajili ya mtu mmoja mmoja kuweka akiba ya fedha zake na kupata riba kutokana na kiasi cha fedha walichonacho kwenye akaunti zao. Akaunti hii inaweza kutumika kuhifadhia fedha kwa ajili ya matumizi maalum au kwa malengo ya muda mrefu huku ikiwa inapata riba ya fedha zilizopo kweye akaunti. Katika akaunti hii, kuna aina mbili za akaunti, Akaunti ya Akiba 1 na Akaunti ya Akiba 2.
Akaunti ya Akiba 1-
• Kiwango cha chini cha kufungulia akaunti ni shilingi 5000. Kiwango cha kuweka kila mwezi kisipungue shilingi 2000
• Akiba itakayozidi shilingi 10000 itapata riba ya asilimia 3kwa mwaka
• Mmiliki wa akaunti hii atapatiwa mkopo usiozidi aslimia 80ya akiba yake kwa muda wowote.

Akaunti ya Akiba 2-
• Kiasi cha chini cha kufungua akaunti kisipungue shilingi 10000
• Akiba ya zaidi ya shilingi 50000 itapatiwa riba ya asilimia 3 kwa mwaka
• Mmiliki wa akaunti anaruhusiwa kuweka au kutoa fedha kwa muda wowote

• Akaunti ya Uwekezaji (Fixed Account)
Hii ni akunti ya kuwekeza ambapo kiwango cha kuanzia ni shilingi 50,000 na riba inaanza kupatikana kuanzia miezi 3, 6 na 12 kwa riba ya aslilimia 3, 4 na asilimia 5 kwa mwaka kwa kufuatana.

• Akaunti ya Mkopo
Benki ya Jumuiya ya Meru hutoa mikopo kwa watu tofauti, vikundi, mikopo ya biashara ya pikipiki (boda boda) na kampuni kwa viwango vya kawaida vya riba rahisi.

• Akiba za Jumuiya
Hii ni akaunti maalum kwa ajili ya vikundi vidogo vidogo kama vyama vya kuweka na kukopa, taasisi zisizo za kiserikali na kadhalika. Kiwango cha chini cha kufungua akaunti ni shilingi 20,000. Akiba ya zaidi ya shilingi 50,000 itapata kiwango cha riba cha asilimia 3 kwa mwaka.

BENKI YA POSTA TANZANIA

Benki hii ilianza shughuli zake rasmi tarehe 1 Machi, 1992 kama chombo kisichokuwa chini ya utawala wa Shirika la Posta na Simu la Tanzania lkwa wakati huo. Ni benki iliyokuwa na Bodi ya Wakurugenzi na utawala unaojitegemea. Benki hii ilianzishwa kama mrithi wa Benki ya Akiba ya Posta iliyoanzishwa kwa mujibu wa Agizo la Serikali la Benki ya Akiba ya Posta la Mwaka 1925. Ilianza shughuli zake mnamo mwaka 1927.

Uanzishwaji wa benki hii uliendana na utambuzi wa serikali kuhusu nguvu zake hasa fursa kubwa ya ushawishi kwa umma, iwe mijini au vijijini.

1. HUDUMA ZA KIBENKI
• Akaunti ya WADU
Ni akaunti inayohusisha mpango wa kuweka akiba kwa mwezi kutokana na mapato anayopata mteja katika shughuli zake kama kuajiriwa au ajira binafsi lengo likiwa ni kuwezesha kufanikisha malengo fulani aliyojiwekea mteja. Kipindi cha kuweka akiba kinaweza kuwa miezi 3, 6, 9, 12 au 24 baada ya hapo mteja anaruhusiwa kutoa kiasi cha fedha au fedha yote huku ikiwa na riba ya kuvutia.
Mahitaji ya kufungua Akaunti
• -Kiasi cha kuanzia ni shilingi 10,000
• -Picha 3 za ukubwa za paspoti za karibuni
• -Kitambulisho cha kazi kwa mwajiriwa na barua kutoka kwa mwajiri au kitambulisho cha kura na barua kutoka kwa Katibu Kata kwa waliojiajiri wenyewe.
2. Mikopo
Benki ya Posta Tanzania inatoa aina mbali mbali za mikopo kulingana na muda au masharti. Muda wa mkopo wa muda mfupi kwa muda usiozidi miezi 24 au kwa muda wa kati kwa mkopo usiozidi miezi 60. Ifuatayo ni mikopo inayotolewa na Benki ya posta:
• Mikopo ya Biashara/Wajasiriamali hutolewa kwa wateja wenye biashara ili kuongeza mitaji ya biashara zao
• Mikopo ya Matumizi ambapo mikopo hii inalenga kuwasaidia waajiriwa kukopa na kulipa mikopo yao kwa kutumia mishahara yao na dhamana kama ardhi au gari haihitajiki ili kupata mikopo ya namna hii
• Mikopo kwa Biashara ndogondogo ni mikopo maalum kwa wafanyabiashara wadogo sana kuendeleza biashara zao ndogo ndogo
• Dhamana ya Benki ni huduma inayopatikana kwa ajili ya wateja ili kuwawezesha kufanya shughuli zao za makubaliano ya kibiashara na ipo mikopo ya aina nne ambazo ni:
i. Udhamini wa Benki
ii. Udhamini wa nyaraka
iii. Udhamini wa nyaraka za utendaji
iv. Barua ya Mkopo
• Mikopo Binafsi ni mikopo inayolenga kusaidia mtu mmoja mmoja kulipia mahitaji yake tofauti kama vile ada za shule, matibabu na maboresho ya nyumba
• Mikopo dhidi ya kufilisiwa mali yako ni aina ya mikopo itolewayo kwa wateja ambao wana akaunti kama WADU na kadhalika.

Kwa maelezo zaidi soma hapa

BENKI YA MAENDELEO

HUDUMA
1. HUDUMA ZA KIBENKI
• Kufungua Akaunti
Benki hii inatoa huduma ya kufungua akaunti kwa ajili ya kuweka akiba kwa mtu mmoja mmoja au vikundi.

2. Mikopo
• Mikopo ya Vikundi Vidogovidogo/ Wajasiriamali
– ¬-Kikundi kiwe na uzoefu wa kibiashara angalau kwa miezi sita
– -Kikundi kiwe na uzoefu wa kukopesheka
– -Eneo la biashara ya kikundi
– -Nyaraka muhimu kuhusu urasmishwaji wa biashara ya kikundi kama vile cheti cha namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) na nyaraka nyinginezo

Kwa maelezo zaidi soma hapa

MAWASILIANO YA TAASISI ZA KIFEDHA