Ijue Biashara inayomilikiwa na Mtu Mmoja

Ziko aina nyingi za muundo wa biashara ambazo unaweza kuzifikiria. Aina mojawapo iliyozoeleka sana hapa nchini ni biashara inayomilikiwa na mtu mmoja.

Biashara inayoendeshwa na mtu binafsi peke yake, au Mfanyabiashara pekee ni aina ya biashara ambayo inamilikiwa na kuendeshwa na binadamu mmoja, na ambapo hakuna tofauti kisheria kati ya mmiliki wa biashara na biashara yenyewe.

Biashara hii inaweza kuendeshwa kwa jina la mmiliki au jina jingine lisilo lake. Itakapotumia jina jingine ambalo sio la mmiliki litakuwa jina tu la biashara, ila halitabadilisha ukweli kuwa hamna taasisi inayotambulika na inayojitofautisha kisheria kati ya mmiliki biashara na biashara yenyewe..

Biashara ya aina hii imejipatia umaarufu mkubwa sana kutokana na urahisi wake, haswa katika uanzishaji, pamoja na gharama ndogo. Mfanyabiashara anahitaji tu kujisajili au kusajili jina lake na kupata leseni na hivi hutosha kuanza kufanya biashara.

Hasara kubwa ya kipekee ya aina hii ya muundo wa biashara ni kuwa mmiliki anabeba majukumu kwa madeni yote ya biashara yake. Hivyo ikiwa atapata matatizo ya kifedha, wadeni wanaweza kufungua kesi/ madai dhidi yake na yakifanikiwa yeye binafsi atawajibika kulipa madeni hayo kutoka kwenye vyanzo binafsi vya fedha.

Faida za biashara ya mtu mmoja

Ni namna rahisi sana kuanzisha na kuendesha biashara

Mmiliki anakuwa mmoja (ama pamoja na waajiriwa au pasipo waajiriwa)

Mmiliki ana mamlaka kamili juu ya maamuzi yote ya kiutendaji na kisera

Matumizi ya faida yote ni juu ya uamuzi binafsi wa mmiliki bila kuingiliwa na mtu yeyote

Hasara za biashara ya mtu mmoja

Muendelezo wa biashara unaathiriwa na kifo, ulemavu, au kuondoka kwa mmiliki

Mmiliki anawajibika binafsi kwa madeni na kodi zinazodaiwa katika biashara yake

Maamuzi yote ya kiutendaji – kuajiri, sera, matatizo, n.k. yanafanywa na mmiliki peke yake

Inaweza kuwa ngumu kupata mtaji (hii inategemea historia ya kibenki ya mmiliki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *