Bima kwa wajasiriamali wadogo na wa kati

Bima ndio njia pekee inayoweza kuikinga biashara yako na majanga mbali mbali

Baada ya kuweka juhudi nyingi katika kuanzisha biashara yako, kukuza biashara yako na kuvutia wateja ni vyema sasa kujikita katika kuilinda dhidi ya majanga mbali mbali ya asili na yanayosababishwa na binadamu.

Bima ndio njia pekee inayoweza kuikinga biashara yako na majanga mbali mbali

Katika ukurasa huu tutajifunza aina za bima kwa wajasiriamali na umuhimu wa kuwa na bima kwa ajili ya biashara yako.

Bima ni mabadilishano kama fidia kati ya mmiliki wa biashara na kampuni ya bima katika kiwango maalumu kwa muhula/kipindi maalumu. Kulipia bima kwa biashara yako ni kuikinga biashara yako isiingie katika hasara endapo tatizo lolote lisilotarajiwa kama vile moto, wizi au majanga ya asili yatatokea. Biashara inapokatiwa bima, wakala wa bima atafidia hasara itakayotokea iwapo biashara itakumbwa na majanga.

Faida ya Bima

 • Usalama dhidi ya matukio yasiyotarajiwa kama vile wizi na moto

Mfanyabiashara anaweza lipia bima biashara yake ili asidhurike na madhara kama vile wizi na moto. Kwa maana hiyo, mhusika hupata fidia yote baada ya kutokea tukio hilo.

 • Njia rahisi za fidia ya hasara endapo bahati mbaya inakutokea

Mtu anaweza lipia bima ya biashara yake ili asidhurike hasara ikitokea. Kama biashara imelipiwa bima, baadhi ya hasara zaweza kulipwa/kufidiwa na hivyo kuwezesha kuendelea kuwepo wa biashara husika.

 • Bima yatoa fursa katika huduma bila kulipia fedha halisi kwa wakati husika, kwa mfano, bima ya afya

Hii ni kwa ajili ya aina zingine za bima kama vile bima ya afya. Mtu hupata fursa kamili kwa ajili ya huduma za afya bila kulipa hata senti. Hapa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wanaweza kuwa na uhakika wa usalama kwa afya zao na za familia zao pindi wanapougua.

 • Huruhusu ukuaji wa biashara kwa urahisi bila kudhurika na changamoto

Katika hili, biashara inaweza kushamiri bila kuwa na wasi wasi kuhusu changamoto zisizotarajiwa zikitokea wakati biashara imelipiwa bima

Mambo ya kuzingatia wakati wa mahitaji ya bima kwa ajli ya biashara

 1. Aina ya bima ambazo mtu anaweza kujiunga

Kuna aina nyingi za bima, kwa mfano, bima ya moto, bima ya wizi na bima ya magari. Ni budi mtu akajua aina mahsusi ya bima ambayo anata kujiunga nayo.

 1. Uhalisi wa kampuni ya bima

Katika maeneo mengi, kuna mawakala wa bima bandia. Kwa hiyo, kabla mtu hajalipia huduma ya bima, Ni budi awe na ufahamu wa uhalisi wa kampuni ya bima. Mambo/masula ya kuzingatia kutambua uhalisia wa kampuni:

 1. Nyaraka zilizothibitishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wakala wa Usajili wa Leseni(BRELA)

 2. Ofisi na maeneo halisi ya kampuni

 3. Nakala za risiti (hata hivyo, hizi zisiwe uthibitisho pekee kwani wakati mwingine zinaweza kuwa za kughushi)

 4. Orodha ya makampuni nchini au orodha ya makampuni ya biashara nchini ili kuhakikisha kama kampuni inatambulika kisheria

 1. Kulinganisha makampuni kadhaa ya bima ili kubaini kampuni inayotoa huduma zinazofaa katika gharama ambazo waweza kuzimudu

Kutokana na kuwepo makampuni mengi yanayotoa huduma za bima kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati, kabla ya kujiunga na mpango wa kampuni yoyote ya bima, mtu anapaswa kukagua gharama kwa kulinganisha makampuni kadhaa ili kupata huduma itakayofaa na kwa bei ya kuridhisha.

 1. Hakikisha kuwa una nyaraka muhumi

Kimsingi, nyaraka muhimu hutegemea na aina ya mali na huduma ya bima mtu atakayojiunga nayo, kwa mfano,

 1. Nyaraka za usajili na leseni

 2. Hati ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN)

 3. Nyaraka halisi/zilizothibitishwa zinazoonesha umiliki na thamani ya mali/biashara

Angalizo: Nyaraka zinazotakiwa hutofautiana kutegemea na makampuni (Tafadhali angalia orodha ya makampuni iliyoambatanishwa)

 1. Lipia bima kwa vitu muhimu sana katika biashara

Ingawa si wazo jema kuacha kusajili baadhi ya vitu/mali, lakini mara nyingi mtu aanze kusajili vitu/mali muhimu zaidi katika biashara. Kwa mfano, kwa biashara ya vyakula, vitu vya kwanza kulipia bima ni jiko.

 1. Lipia bima dhidi ya majanga yanayoweza kutokea

Japokuwa si rahisi kutabiri kutokea kwa janga, lakini kutegemea na aina ya biashara na eneo biashara itakapofanyika, kuna majanga ambayo mtu anatakiwa kupambana nayo. Kwa mfano katika biashara ya hoteli, moto, na wizi wa mali ni vitu vya lazima kujiunga katika mipango yake wakati mipango ya biashara ya usafirishaji inaweza kuhuisha mali, ajali na wizi.

Aina za msingi za bima kwa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati

 1. Wizi

Aina hii ya bima inahusisha kulipa fidia kwa madhara yanayoweza kutokea baada ya wizi wa mali za biashara

 1. Moto

Hii mtu anaweza kulipia bima ya nyumba na vifaa vyake vya biashara dhidi ya moto

 1. Majanga ya asili

Hii inahusu kulipia biashara kutokana na madhara yanayotokana na majanga ya asili kama vile mafuriko na tetemeko.

 1. Mpango wa Bima ya Afya/Matibabu

Aina hii ya bima inaweza kuwa katika aina mbili zifuatazo:

 1. Aina ya kwanza ya bima ya afya ni kutoa huduma ya afya kwa watu. Katika aina hii ya bima, watu wanaweza kupata huduma za afya baada ya kujiunga na mpango wa bima ya afya.

 2. Aina ya pili ya bima ya afya ni kulipia fidia kutokana na madhara ya aina

yoyote yanayoweza kutokea kutokana na ajali au kifo wakati wa kazi au katika mazingira ya kazi.

 1. Bima ya mali

Katika aina hii ya bima mtu alipie bima ya mali. Kuna aina nyingi zinazoweza kulipiwa bima kama zifuatazo:

 • Mizigo ya bandari: hii inahusisha kinga dhidi ya upotevu wa mizigo wakati inasafirishwa baharini (kwa meli), angani (kwa ndege) au ardhini (kwa barabara au reli).

 • Magari: Sheria inataka magari yote katika barabara za umma kuwa na bima au kinga dhidi ya dhima kwa kuumia kwa mwili na kwa abiria.

ANGALIZO: Biashara yoyote inayoendeshwa nchini kisheria yaweza lipiwa bima

Orodha ya Sheria Zinazoongoza Huduma za Bima

 1. Sheria ya Bima ya mwaka 2009

Sheria iliyoanzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Nchini (Tanzania Insurance Regulatory Authority). Chini ya Sheria hii, mamlaka imepewa nguvu ya kuongoza na kusimamia biashara ya bima na masuala yote yanayohusiana na bima Tanzania Bara na Zanzibar. Sheria hii inaipa mamlaka nguvu ya kusimamia na kuratibu shughuli zote za bima. Sheria hii inaainisha kanuni za maadili kwa ajili ya bima na taarifa zote muhimu za kuendesha biashara ya bima, wakati mamlaka ya usajili wa biashara za bima amepewa Kamishna wa Bima au Naibu Kamishna wa Bima.

Sheria hii inaelekeza kwamba, mtu yeyote atakayeanzisha biashara ya bima lazima awe mkazi wa Tanzania, lakini kama ni kundi angalau theluthi moja ya wajumbe wa bodi wawe ni wakazi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sheria inaelekeza taratibu na nyaraka muhimu za kuanzisha biashara ya bima. Pia inaelekeza haki ya bima ya tatu kama vile kuwa na bima dhidi ya dhima kama kufilisika pamoja na haki ya kupata taarifa kwa mwendesha biashara ya bima.

 1. Kanuni za Bima Ndogo za 2003

Kanuni hizi zinahusu wakala wa bima ndogo na mwekeza bima anayehusika na bima kwa ujumla kuhusu bima ndogo ya mali au ya maisha. Huduma chini ya kanuni hizi zinahusu banda, mifugo, vifaa vya uvuvi, mazao ya kilimo, zana za biashara ndogo au vifaa au ajali ya mtu binafsi au kundi, elimu, muda wa mkopo, maisha ya familia na bima ya mkataba wa mazishi.