Jinsi ya kutengeneza Batiki

MAHITAJI:

1.Vibanio vyenye urembo mbalimbali.

2.Sponji zenye urembo mbalimbali.

3.Brash kubwa/ndogo.

4.Meza kubwa yenye urefu wa mita moja mpaka mbili.

5.Sufuria.

6.Vitambaa vya mpira.

7.Misumari midogo.

8.Jiko.

MADAWA:

1.Sodium hydrosulphate.

2.Caustic soda

3.Mshumaa.

KAZI ZAKE:

1. Sodium hydrosulphate ni kuimarisha rangi isichuje,kama itachanganywa na caustic soda.Madawa haya huwa kazi yake ni moja lakini ikikosekana moja nyingine haifanyi kazi.

2. Kazi ya mshumaa ni kuweka urembo kwenye nguo au kwenye vitambaa kwa kutumia vibao au sponji zenye urembo wa tembo,twiga,matunda au aina yoyote ya urembo unayotaka mtengenezaji.

JINSI YA KUTENGENEZA.

(a) JINSI YA KUGONGA MISHUMAA:

Chemsha mshumaa uchemke sawasawa kisha ipua upoe kidogo. Andaa kitambaa cha pamba (cotton) na kukitandika mezani, chovya kibao chenye picha kwenye mshumaa kisha gonga kwenye kitambaa na kuacha nafasi kidogo. Endelea kugonga picha hizo mpaka kitambaa kiishe.

(b) JINSI YA KUWEKA RANGI:

Chemsha maji ya moto yachemke sawa sawa kisha pima lita tano mpaka sita. Baada ya hapo pima caustic soda vijiko3 na sodium hydrosulphate vijiko vinne mpaka vitano. Changanya na maji ya moto,weka rangi kijiko kimoja. Baada ya hapo pima maji lita kumi na tano na changanya na mchanganyiko wa madawa ili maji yawe vuguvugu. Tumbukiza vitambaa vya vinne vya mita tatu kwa wakati mmoja na kuvigeuzageuza viingie rangi kwa dakika kumi mpaka kumi na tano. Suuza kwa maji baridi na uanike kwenye kivuri ili mshumaa usiyeyuke.

(c) KUWEKA RANGI YA PILI:

Katika kuweka rangi hii kinachofanyika ni kuongeza vipimo vya ranagi tu. Ongeza vipimo vya rangi viwili na zaidi ya mala ya kwanza,maji,mudani uleule,

Weka mshumaa sehemu ambayo haina mshumaa kwa kutumia urembo uleule.Pima rangi kwa kufuata hatua zilezile. Tumbukiza vitambaa vitatu,geuza kwa mda uleule kisha anika.

(d) JINSI YA KUTOA MSHUMAA:

Chemsha maji yachemke vizuri,changanya na sabuni ya unga jikoni,tumbukiza kitambaa kimoja kimoja jikoni ili kutoa mshumaa,geuza kwa mti,suuza kwenye maji ya baridi yaliyochanganywa na maji.

PIGA PASI TAYARI KWA KUUZA.

Imeandaliwa na 0654627227

mdeonidas@yahoo.com

Jinsi ya kutengeneza Chaki

MARIGHAFI;

CHOKAA NYEUPE.

MAJI

RANGI(Kama unahitaji iwe ya rangi)

FOIL PAPER(MAUMBO)

MOTO

HATUA ZA KUTENGENEZA.

Chukua chokaa kilo moja iliyochekechwa na kupata unga ulio safi,maji lita moja,rangi 10mls.Changanya mchanganyiko huu kwa pamoja upate uji mzito na ukoroge kwa dakika kumi na tano.

HATUA YA PILI.

Weka mchanganyiko wako katika maumbo yako ya vibox au bati ambazo zimekatwa katika shape unayoitaka.

Weka juani chaki zako mpaka zikauke.

Zitoe kwenye maumbo uziweke jikoni na kuzichoma kama unavyochoma matofari au vyungu mpaka ukiishika uone inatoa vumbi na ukiidondosha ikatike vipande viwili au zaidi.

Chaki zako tayari

VIFUNGASHIO NA LEBO

 • Fungasha chaki kwenye chombo kinachofaa
 • Bandika lebo kwenye chombo kifungashio kuhusu bidhaa: Aina ya chaki, uzito, maelekezo ya matumizi na uhifadhi na mchanganyiko wa madawa, jina la mtengenezaji, anwani, namba ya simu na barua pepe
 • Onyesha nembo za ubora kama TBS na GS1 (Barcode)

HATI NA VIBALI

 • Onana na mamlaka husika kupata vibali na vyeti: TBS and GS1
 • Pata hati ya TCCIA kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi
 • Fuata taratibu za uuzaji bidhaa nje ya nchi

Mapishi ya Keki

Mahitaji

720 gram unga wa ngano

1 kijiko kidogo cha chai Baking powder

1 kijiko kidogo cha chai chumvi

360 gram sukari

1 kijiko kidogo cha chai  unga wa Cinnamon (Mdalasini)

4 mayai vunja na ubakize ute mweupe tu

180 gram ndizi ya kuiva iponde ponde

120 gram Vegetable Oil

480 gram ndizi mbivu kata kata vipande

1 kijiko kidogo cha chai Vanilla Essence

120 gram kata kata vipande vya nanasi

240 gram vunja vunja koroshon za kuokwa

Muda wa maandalizi : saa 1 mpaka 2

Muda wa kupika : dakika 30 mpaka saa 1

Idadi ya walaji : 8 na zaidi

Katika bakuli changanya unga wa ngano, chumvi, sukari, baking powder na unga wa mdalasini ( cinamon) Changanya vizuri mpaka vichanganyike kabisa

Chukua bakuli kisha piga ute mweupe wa yai na uchanganye na mafuta, vanilla pamoja na ndizi ya kuiva ulio iponda ponda kisha mimina mchanganyiko huu katika unga wako.

Tumia mwiko kuchanganya mchanganyiko huu pole pole mpaka uchanganyike.

Baada ya hapo weka vipande vya nanasi ulivyo kata kata, 240 gram ya korosho zilizookwa pamoja na vipande vya ndizi mbivu.

Endelea kuchanganya kwa kutumia mwiko mpaka upate mchanganyiko safi kabisa.

Chukua vyombo vya kuokea keki vyenye vya mduara na kina cha 9-inch  kisha mimina mchanganyiko wako sawa kwa sawa katika vyombo vyote vitatu.

Coma keki yako katika moto wa 350° kwadakika 25 mpaka 30 inategemea na oven yako pia unaweza choma mpaka ukiweka katika keki tooth pick na inatoka kavu. Poza keki zako katika wire racks kwadakika 10; kisha toka katika pans ilizo chomea, na kisha ziache zipoe moja kwa moja katika wire racks.

Kwajili ya kupambia: Piga cream cheese pamoja na  butter kwa speed ndogo kwama unatumia mashine ya umeme mpaka ilainike kabisa.

Pole pole na kidogo kidogo mimina icing sugar, endelea kupiga kwa speed ndogo mpaka iwe nyepesi na inapanda Kisha ongezea vanilla.

Paka mchanganyiko wako wa Cream Cheese katika kila keki yako kwa upande wa juu tu

Kisha zipandanishe na juu kabisa paka tena kama ionekanavyo katika picha Kisha paka na pembeni ya keki pia kama picha inavyoonyesha iwe rafu rafu tu Kisha mwagia juu ya keki yako 120 gram cup za korosho zilizookwa na ukazikata kata.

Kisha iweke keki yako katika friji. Ladha ya ndizi mbivu na nanasi pamoja na korosho inafanya keki hii iwe na ladha ya kipekee na ukiila mara moja utatamani kula kila siku!

Huu ni muonekano wa keki ikikatwa kwa ndani unaona mpangiliona muonekano wake  ulivyosafi?

Jinsi ya Kutengeneza mishumaa

MISHUMAA

Malighafi na Vifaa

 1. Mafuta ya taa waxi/ Nta (Paraffin wax)
 2. Asidi boriki na Stearine 
 3. Rangi (ukipenda)
 4. Pafyumu (ukipenda)
 5. Utambi / uzi
 6. Umbo (mould) ya mshumaa
 7. Jiko  la  mafuta  ya  taa/ mkaa na sufuria na vijiko vya chakula
 8. Vifungashio vyenye lebo

Utengenezaji

Utambi

 • Changanya asidi boriki vijiko 5 vya chakula na maji vijiko 4 vya chakula
 • Koroga kwa dakika 5
 • Tumbukiza utambi ukae kwa dakika 5
 • Anika ukauke

Mshumaa

 • Andaa maumbo  ya mshumaa
 • Weka utambi katikati ya chombo kwa kushikiza na ute wa mshumaa na funga utambi
 • Weka sufuria jikoni, changanya nta kilo 1, stearine vijiko 4, chemsha   
 • Changanya rangi, parfyumu, asidi na koroga hadi mchanganyiko uyeyuke
 • Epua, mimina mchanganyiko kwenye maumbo na weka kwenye kivuli hadi mchanganyiko unaganda
 • Ondoa mshumaa taratibu kutoka kwenye maumbo

Vifungashio na lebo

 • Fungasha mishumaa kwenye chombo kitakachomvutia mteja aweze kununua
 • Bandika lebo kwenye chombo kuhusu bidhaa: Aina, mchanganyiko wa malighafi, uzito au idadi, maelekezo ya matumizi na uhifadhi, jina na anwani ya mtengenezaji, namba ya simu na barua pepe
 • Onyesha nembo za ubora kamaTBS na GS1 (Barcode)
 • Fuata maelekezo na taratibu za TBS

Hati na vibali

 • Onana na mamlaka husika kupata vibali na vyeti: TBS and GS1
 • Pata hati ya TCCIA kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi
 • Fuata taratibu za uuzaji bidhaa nje ya nchi

Achali ya Embe/Mango pickle

Malighafi

 1. Embe, nyanya na vitunguu 2 vikubwa (Embe bichi au lililoiva?)
 2. Chumvi
 3. Siki kijiko 1  cha  chai 
 4. Viungo na mafuta ya kula
 5. Maji  ya  limao 
 6. Vifungashio: chupa. mifuniko, lebo mbalimbali

Utengenezaji

 • Osha vizuri embe
 • Kata embe vipande  vidogovidogo bila  kugusa  kokwa
 • Weka vipande  kwenye  kichanja na  anika juani kwa muda wa nusu  saa
 • Hifadhi  embe kwenye  chombo  kwa siku tano
 • Menya nyanya robo  kilo na katakata vipande vidogo
 • Katakata  vitunguu
 • Andaa maji ya limao vijiko 2  vya  chai na siki kijiko  1  cha  chai 
 • Tengeneza rosti  ya  mchanganyiko  wa  malighafi  zote ulizoandaa
 • Changanya vipande  vya  embe na rosti
 • Weka chumvi vijiko 2 vya chai
 • Hifadhi  kwa  ajili ya matumizi au kupeleka sokoni

Vifungashio na lebo

 • Fungasha bidhaa yako kwenye chombo kitakachomvutia mteja aweze kununua
 • Bandika lebo kwenye chombo kuhusu bidhaa: Aina na jina, uzito, mwisho wa matumizi, maelekezo ya matumizi na uhifadhi, mchanganyiko wa malighafi, jina la mtengenezaji na anwani, namba ya simu na barua pepe
 • Onyesha nembo za ubora kamaTBS, TFDA na GS1 (Barcode)
 • Fuata maelekezo na taratibu za TBS na TFDA

Hati/vyeti na vibali

 • Onana na mamlaka husika kupata hati na vyeti: TFDA, TBS and GS1
 • Pata hati ya TCCIA kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi
 • Fuata taratibu za uuzaji bidhaa nje ya nchi

Tomato Sauce

Utangulizi
Sosi ya nyanya ni kiungo kinachotumika ili kukoleza chakula wakati wa mlo. Sosi ya nyanya hutengenezwa kutokana na nyanya zilizoiva na ni viungo.

Jinsi ya kutengeneza:
Vifaa vinavyohitajika:
 Mashine ya kusagia
 Sufuria ya kuchemshia
 Mzani
 Vifungashio:- Chupa za sosi zenye mifuniko
– Lebo na ‘seal’

 Mahitaji:
1. Nyanya zilizoiva gramu 900
2. Siki (vinegar) mls 50
3. Sodiumu Benzoate
4. Maji salama
5. Vitunguu maji, vitunguu swaumu, hoho ya unga, haradani (mustard n.k)
6. Chumvi
7. Sukari
8. Unga wa muhogo 1-1.3%

Hatua za Utengenezaji:
 Chagua nyanya zilizoiva vizuri zenye umbo la yai- nyanya za Tengeru ni nzuri zaidi.
 Osha kwa maji safi
 Menya na kuondoa mbegu (waweza pia pika na mbegu ingawa kuna wengine huwa hawapendi ladha na muonekano wa mbegu kwenye sosi)
 Katakata vipande vidogo na weka kwenye chombo cha kusagia.
 Saga vizuri kupata rojo
 Visage viungo( vitunguu, hoho, pilipili manga, vitunguu swaumu, binzari n.k kulingana na matakwa) na vifunge kwenye kitambaa safi.
 Kitumbukize kwenye maji kiasi na chemsha na kamua kitambaa ili kupata supu
 Changanya supu ya viungo, chumvi, sukari na mchanganyiko wa nyanya Chemsha mpaka upate uji mzito. Mara nyingi sosi inakua tayari iwapo uzito umebaki nusu ya uzito wa mchanganyiko wa awali.
 Ongeza kamikali (Sodium Benzoate, Vinegar) kisha chemsha kwa dk 5
 Paki kwenye vifungashio safi ikiwa bado ina joto nyuzijoto 80-90

Vifungashio na lebo

 • Fungasha bidhaa yako kwenye chombo kitakachomvutia mteja aweze kununua
 • Bandika lebo kwenye chombo kuhusu bidhaa: Aina, uzito au ujazo, mwisho wa matumizi, maelekezo ya matumizi, uhifadhi na mchanganyiko wa malighafi/lishe, jina na anwani ya mtengenezaji, namba ya simu na barua pepe
 • Onyesha nembo za ubora kama TBS, TFDA na GS1 (Barcode)
 • Fuata maelekezo na taratibu za TFDA na TBS

Hati na vibali

 • Onana na mamlaka husika kupata vyeti: TFDA, TBS and GS1
 • Pata hati ya TCCIA kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi
 • Fuata taratibu za uuzaji bidhaa nje ya nchi