Kuongeza muda wa kuhakiki taarifa za TIN

kayombo

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo akizungumza jambo. TRA imeongeza mwezi mmoja ili kuwapa mda zaidi wakazi wa Dar es Salaam kuhakiki taarifa za TIN

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza kuongeza mda wa kuhakiki na kuboresha taarifa za Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN).

Kwa sasa uhakiki wa TIN utaendelea hadi tarehe 30 Novemba 2016.

“Wananchi wote wenye TIN- katika Mkoa wa Dar es Salaam wanatakiwa kufika katika vituo vilivyoainishwa ili kuboresha na kuhakiki taarifa zao kabla ya tarehe ya mwisho kwa maana muda hautaongezwa tena,” wanasema TRA.

Wale wote watakaoshindwa kuhakiki au kuboresha taarifa zao, TIN zao za zamani zitafungwa na kuondolewa kwenye mfumo hivyo hawataweza tena kutumia namba hizo.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA ZOEZI LA UHAKIKI
1. Wenye TIN za biashara wanatakiwa kuboresha au kuhakiki taarifa katika ofisi za Mikoa ya kodi ziliposajiliwa biashara zao katika vituo vifuatavyo:-

Mkoa wa Kodi Ilala: Jengo la Mariam Tower (Shaurimoyo) na 14Rays (Kariakoo-Gerezani)

 Mkoa wa Kodi Kinondoni: Jengo la LAPF (Kijitonyama) na Kibo Complex (Tegeta)

 Mkoa wa Kodi Temeke:Uwanja wa Taifa

Ofisi za TRA Kigamboni

Ofisi za TRA Mbagala

2. Wenye TIN zisizo za biashara wanaweza kuboresha au kuhakiki taarifa zao katika ofisi yoyote ya TRA ya Mkoa au wilaya iliyo karibu nae.

3. Fomu za kujiandikisha au kuhakiki taarifa zinapatikana ofisi zote za TRA na kwenye Tovuti yetu ya TRA na zinaweza kujazwa na kuwasilishwa kwa mkono katika katika vituo vya uhakiki zikiwa na viambatisho vifuatavyo:

(i) Kitambulisho (Kitambulisho cha kupigia kura au cha taifa, au leseni ya udereva)
(ii) Mkataba wa pango au leseni ya Makazi kama unamiliki jengo la biashara.
(iii) Cheti cha kuandikishwa cha Kampuni kutoka BRELLA (Certificate of Incorporation) – Kwa Makampuni tu.
(iv) Nyaraka za muundo na dhumuni la uanzishwaji wa kampuni(Memorandum and Article of Association)-Kwa Makampuni tu
(v) Cheti cha TIN.

4. Mlipakodi atatakiwa kufika yeye mwenyewe ili kuhakiki alama za vidole zilizo kwenye mfumo.

Kwa taarifa zaidi bonyeza hapa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *