Utangulizi

Kuwa mmiliki wa biashara ndogo kunaambatana na changamoto mbalimbali ambazo zinaendana na ukubwa na shughuli za biashara yenyewe. Mmiliki analazimika kukabili changamoto hizo, zikiwemo za uuzaji, usambazaji, usimamizi wa fedha na kuhakikisha biashara inakua. Haya yote anayafanya huku akiwa na wafanyakazi wachache, au pengine bila kuwa na hata mmoja.

Katika kujaribu kufanikisha, anakabiliwa pia na changamoto muhimu ya kufanya shughuli za kiutawala. Utawala wenye ufanisi katika biashara unaleta matokeo mazuri kwa mfanyabiashara binafsi na ustawi wa biashara yake pia. Ni muhimu kufanya yafuatayo kuhakikisha unafanya baishara yako kwa mujibu wa kanuni na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Sajili jina la biashara yako

Kabla ya kufanya taratibu nyingine zozote, mjasiriamali atatakiwa kusajili jina la biashara. Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) ndio inajukumu la kusajiri majina yote ya biashara nchini.

Utatakiwa kuwasilisha kwa Brela mapendekezo ya majina matatu ya biashara yako. Lengo la kupeleka majina matatu ni kuhakikisha kuwa angalau jina moja kati ya hayo matatu haliingiliani na majina mengine ambayo tayari yalishasajiliwa. Kwa hiyo ikiwa jina la kwanza ulilopendekeza litaingiliana na lililosajiliwa tayari mamlaka itasajili jina la pili na kama nalo litapatikana lipo tayari pendekezo la tatu ndio litasajiliwa.

Gharama za kusajili jina la biashara kwa mujibu wa Brela ni Shilingi 20,000 na usajili unaweza ukafanyika pia kwa njia ya mtandao.

Maelezo zaidi ya namna ya kusajili jina la biashara yanapatikana katika tovuti ya Brela, kwa kufika katika ofisi zao zilizopo Dar es salaam na Mwanza au kupitia mawakala wao.

Jisajili na Mamlaka ya Mapato

Mara biashara au kampuni inapokamilishwa kusajiliwa na msajili wa makampuni, inalazimika kusajiliwa na ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyo karibu. Hati ya kwanza unayopaswa kupewa na Mamlaka ya Mapato ni namba ya utambulisho ya mlipakodi (TIN). Kwa kawaida namba hii inapatikana ndani ya siku tatu.

TIN inapotolewa, jalada la kodi linafunguliwa. Namba ya jalada inapotolewa, kampuni inategemewa kujaza fomu ya muda (ya makadirio) ya taarifa za kodi ya mapato. Fomu hizi za muda zinapaswa kuwasilishwa ndani ya miezi mitatu tangu kuanza kwa biashara. Kampuni inatakiwa kukadiria faida yake kwa mwaka wa kwanza na kulipa kodi kwa makadirio hayo mara nne kwa mwaka. Kingine kinachotolewa TRA baada ya namba ya jalada kupatikana ni cheti cha kukamilisha hatua za awali za kodi, ambacho kinaweza kutumika kupata leseni ya biashara.

Ikiwa mauzo ya biashara kwa mwaka ni kuanzia shilingi milioni mia moja, biashara hiyo inalazimika pia kujisajili kwa ajili ya kodi ya ongezeko la thamani (VAT). VAT inatozwa katika kiwango cha 18% ya mauzo. Ili kujisajili kwa ajili ya VAT, mwombaji anapaswa kujaza fomu ya maombi inayopatikana katika idara ya VAT ya TRA. Fomu inapaswa kukamilishwa na kurejeshwa pamoja na nakala ya nyaraka zifuatazo:

 • Cheti cha usajili cha kampuni (kwa kampuni) au cheti cha usajili (kwa biashara zinazomilikiwa kwa muundo wa ubia au kumilikiwa na mtu mmoja pekee);
 • Mkataba wa kuanzisha kampuni na sheria za ndani za kampuni, ambavyo vinaonesha, pamoja na mambo mengine, iwapo malengo ya kampuni yaliyotajwa katika mkataba wa kuanzisha kampuni yanairuhusu kamouni kufanya shughuli ambazo zinaombewa leseni.;
 • Ushahidi wa uraia wa Tanzania, kwa mfano nakala ya hati ya kusafiria, cheti cha kuzaliwa, au kwa ambaye sio raia, kibali cha kuishi nchini cha daraja A (kinachoonesha kuwa mwenye kibali ni mwekezaji kwenye kampuni/ biashara hiyo);
 • Ikiwa wanahisa wa kampuni sio raia na hawana vibali vya kuishi nchini, hati ya kiapo ya raia/ mkazi inapaswa kuwasilishwa;
 • Ushahidi kuwa mwombaji ana eneo linalofaa kwa ajili ya biashara anayoiombea leseni. Ushahidi ambao unaweza kuwasilishwa ni hati ya ardhi, mkataba wa pango, stakabadhi ya kulipa pango, au stakabadhi ya kulipa kodi ya ardhi au pango;
 • Namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania;
 • Cheti cha kukamilisha hatua za awali za kodi kilichotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (idara ya kodi ya mapato);
 • Leseni ya biashara iliyotolewa na wizara ya viwanda na biashara au mamlaka ya serikali za mitaa, chini ya sheria ya leseni za biashara; and
 • Picha tatu za mwombaji, au mmoja wa wakurugenzi wakazi wa kampuni au mwakilishi ambaye yupo nchini.

Kupata vibali/ leseni za biashara

Aina na idadi ya vibali/ leseni zinazohitajika hutofautiana kati ya sekta moja na nyingine, kutegemeana na kiwango cha udhibiti katika sekta husika. Kiujumla inashauriwa kutafuta ushauri wa kisheria kuhusu vibali vinavyohitajika katika sekta unayokusudia kuingia. Pamoja na kukidhi matakwa ya sekta husika, kila biashara inapaswa kupata leseni ya ‘jumla’, inayotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Leseni za Biashara ya mwaka 1972. Ili kupata leseni ya jumla ya biashara, mwombaji analazimika kuwasilisha nyaraka zifuatazo:

 • Vivuli ya cheti cha usajili wa kampuni a cheti cha kufuata sharia (kwa makampuni) au cheti cha usajili (kwa biashara zinazomilikiwa na mtu binafsi au kwa ubia);
 • Mkataba wa kuanzisha kampuni na sheria za ndani za kampuni, ambavyo vinaonesha, pamoja na mambo mengine, iwapo malengo ya kampuni yaliyotajwa katika mkataba wa kuanzisha kampuni yanairuhusu kamouni kufanya shughuli ambazo zinaombewa leseni.;
 • Ushahidi wa uraia wa Tanzania, kwa mfano nakala ya hati ya kusafiria, cheti cha kuzaliwa, au kwa ambaye sio raia, kibali cha kuishi nchini cha daraja A (kinachoonesha kuwa mwenye kibali ni mwekezaji kwenye kampuni/ biashara hiyo);
 • Ikiwa wanahisa wa kampuni sio raia na hawana vibali vya kuishi nchini, hati ya kiapo ya raia/ mkazi inapaswa kuwasilishwa;
 • Ushahidi kuwa mwombaji ana eneo linalofaa kwa ajili ya biashara anayoiombea leseni. Ushahidi ambao unaweza kuwasilishwa ni hati ya ardhi, mkataba wa pango, stakabadhi ya kulipa pango, au stakabadhi ya kulipa kodi ya ardhi au pango
 • Namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania;

Kama ilivyodokezwa awali hapo juu, yapo pia masharti ya nyongeza ili kupata mamlaka kutoka vyombo vya udhiibiti vya kisekta. Ukitujulisha kuhusu biashara yako ni rahisi kukushauri kuhusu masharti yaliyopo mahsusi katika sekta inayohusika na biashara yako. Ifuatayo ni mifano ya matakwa mahsusi ya sekta:

 • Leseni ya uwakala wa forodha (inayotolewa na TRA) kwa wanaotaka leseni ya kuendesha biashara ya uwakala wa forodha (kusafirisha mizigo nje ya nchi na kutoa mizigo inayoingia nchini.
 • Leseni ya wakala wa utalii (inayotolewa na wizara ya maliasili na utalii) kwa waombaji wa kibali cha kufanya biashara za utalii kama vile hoteli ya kitalii, wakala wa usafirishaji, uwindaji, uongozaji wa watalii, n.k.
 • Kibali cha utafutaji/ uchimbaji madini (kinachotolewa na wizara ya nishati na madini) kwa waombaji wa leseni za kufanya bishara zinazohusisha uchimbaji madini.
 • Kibali cha mawasiliano/utangazaji/ usambazaji habari (kinachotolewa na mamlaka ya mawasiliano) kwa wale waombaji wa leseni ya kufanya biashara ya utangazaji (redio, TV), mawasiliano ya simu, intaneti, n.k.
 • Leseni ya bima (Inayotolewa na wakala wa usimamizi wa bima) kwa wale wanaoomba kibali cha kuendesha biashara ya bima.
 • Kibali/leseni maalum (kinachotolewa na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania) kwa waombaji wa leseni ya biashara inayojihusisha na chakula, dawa, na vipodozi.
 • Leseni ya uvuvi (inayotolewa na wizara ya maliasili na utalii) kwa waombaji wa kibali cha kuendesha biashara ya uvuvi.
 • Vyeti/ vibali vya kitaaluma, kwa biashara zinazotegemea taaluma kama vile madaktari, wanasheria, marubani, wahasibu, manahodha wa meli, n.k. (hivi hutolewa na taassisi/ bodi za taaluma hizo).
 • Leseni za viwanda (inayotolewa na wizara ya viwanda na biashara), kwa waombaji wa leseni za kuanzisha viwanda.
 • Kwa bishara zinazohusisha kutoa huduma za ulinzi, lazima kibali kitolewe na Mkuu wa jeshi la polisi, chini ya wizara ya mambo ya ndani.

Utaratibu wa kutoa leseni

Sheria na taratibu za kupata huduma za leseni Manispaa ya Ilala