Bei ya Dizeli na mafuta ya taa yashuka

Mamlaka  ya  Udhibiti  wa Huduma  za Nishati  na  Maji  (EWURA), imetangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi Januari 2017.

Kwa mujibu wa bei mpya bei  za  jumla  na  rejareja  kwa  mafuta  ya  aina zote  yaani  Petroli,  Dizeli  na  Mafuta  ya  Taa  zimebadilika  ikilinganishwa na  na bei za mwezi Disemba.

Kwa  Mwezi  Januari  2017,  bei  za  rejareja kwa Dizeli na Mafuta ya Taa zimepungua kwa; TZS 66/lita sawa na asilimia 3.68 na TZS 37/Lita sawa na  asilimia  2.11 sawia, na kwa  mafuta  ya  Petroli bei imeongezeka kidogo  kwa  TZS  0.10/lita  sawa  na asilimia 0.01.

Vilevile,kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita,  bei za jumla kwa mafuta ya  Dizeli na  Mafuta  ya  Taa  nazo    zimepungua  kwa;TZS  66/lita sawa  na  asilimia  3.91na  TZS  37/lita  sawa  na asilimia 2.25, sawia  ambapokwa mafuta ya Petroli bei imeongezeka kidogo kwa TZS 0.01/lita sawa na asilimia 0.01.  Mabadiliko haya yametokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia.

“Hakutakuwa namabadiliko ya bei za mafuta kwa mkoa wa Tanga, hii ni kutokana na kutopokewa mzigo mpya wa mafuta kwenye bandari ya Tanga kwa mwezi wa Desemba 2016. Hivyo bei za mkoa wa Tanga kwa mwezi wa Januari 2017 zitaendelea kuwa kama zilivyokuwa mwezi wa Desemba 2016,” anasema Mkurugenzi wa Ewura Felix Ngamlagosi.

Kwa taarifa kamili bonyeza hapa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *