Mpango mkakati wa kutatua changamoto za ajira kwa Vijana Wazinduliwa

mgomo_mabasi

Takwimu zinaonyesha kuwa idadi kubwa ya vijana katika nchi zinazoendelea kama Tanzania inaendelea kukua kwa kasi sana na hivyo kuongezeka kwa vijana wengi wasio na ajira na wenye hali duni ya maisha, ukosefu wa mitaji, ukosefu wa mbinu jumuishi na kukosa fursa za kiuchumi.

“Ajira Yangu Business Plan Competition” ni mpango mkakati wa kutatua changamoto za ajira kwa Vijana, Tanzania.

Ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili vijana nchini, Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), kwa pamoja wamebuni mpango huu.

Ajira Yangu Business Plan Competition itahusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18-35, wale wanaotaka kuanza biashara au wanaotaka kupanua na kuboresha biashara zao.

Vijana hao watatakiwa kuja na mipango rasimu ya biashara kwaajili ya mashindano katika sekta zifuatazo;

* Biashara ya Kilimo na kilimo usindikaji ikiwa ni pamoja na viwanda

* Biashara inayohusu vyombo vya habari, masoko, mawasiliano, michezo, vifaa, sanaa na utamaduni, utalii na burudani.

* Biashara inayogusa mazingira na utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na biashara ya kijamii.

* Biashara inayohusu habari na mawasiliano, teknolojia ikiwa ni pamoja na usindikaji biashara

Mpango huu umebuniwa kwaajili ya vijana kupata ujuzi wa kuanzisha na kuendeleza biashara na kuwawezesha mitaji, ili waweze kuanza au kuboresha biashara zao, na kutengeneza nafasi za ajira kwao wenyewe na kwa vijana wengine pia.

Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya vijana katika nchi zinazoendelea kama Tanzania inaendelea kukua kwa kasi sana na hivyo kuongezeka kwa vijana wengi wasio na ajira na wenye hali duni ya maisha, ukosefu wa mitaji, ukosefu wa mbinu jumuishi na kukosa fursa za kiuchumi.

Taratibu za Uombaji:

Taratibu za uombaji zitahusisha awamu tatu.

Awamu ya kwanza itahusisha kujaza fomu ya maombi inayopatikana ndani ya tovuti ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC).

Maombi yataanza kupokelewa kuanzia Aprili 18 mpaka Mei 9, 2016.

Awamu ya pili itahusisha mafunzo ya biashara. Vijana ishirini na tano waliochaguliwa kutoka awamu ya ya kwanza watapitia mafunzo ya kina kwa siku moja juu ya mipango ya biashara.

Mafunzo haya yatakuwa kwaajili ya vijana wote ishirini na tano waliochaguliwa ili kunoa ujuzi wao katika mipango ya biashara ambayo itasababisha kuendeleza mipango yao ya biashara.

Matokeo muhimu ya mafunzo hayo, itakuwa ni kwa kila mshiriki kuandaa, kuongeza na kuboresha mpango kamili wa biashara.

Awamu ya tatu ya , Ajira Yangu Business Plan Competition itahitimishwa kwa kuwakutanisha washiriki wote ishirini na tano.

Washiriki ishirini na tano waliochaguliwa watawasilisha mawazo bunifu ya biashara zao mbele ya washauri, majaji, wawekezaji walioalikwa pamoja na wananchi wengine.

Kila mshiriki atapata fursa ya kujieleza kuhusu safari yake ya ujasiriamali na mafanikio yake ya baadaye. Na mchango wa biashara yake katika kujenga ajira kwa wengine.

Baada ya hapo, majaji watachagua mawazo ya biashara iliyo bunifu na yenye uvumbuzi kuliko wote.

Washindi wa Ajira Yangu Business Competition watatangazwa baada ya majaji kupendekeza majina yaliyokidhi vigezo vilivyowekwa.Washiriki wote watapokea msaada wa kiufundi na kitalaamu ili kukuza biashara zao kwa mwaka mmoja.

Washiriki sita wa kwanza wenye mawazo ya ubunifu watachaguliwa na kila mmoja atapokea tuzo kwa njia ya mtaji ili kuwawezesha kuanzisha au kuendeleza biashara zao, na kujenga ajira zao wenyewe na kwa kwa wengine.

Lengo la Ajira Yangu Business Plan Competition ni kuongeza idadi ya vijana wanawake kwa wanaume katika biashara na kuzalisha kazi na ajira.

Kwa Mawasiliano zaidi:

ILO Country Office, Kazi House, P. O. Box 9212, Dar es Salaam, Tanzania.

Tel : +255 22 2196700 | Mobile: +255 763 160186 | Fax : +255 22 2126627 | Email: lazaron@ilo.org

AU

National Economic Empowerment Council, 12 Kivukoni Street, P.O.Box 1734, Dar es salaam, Tanzania.

Phone: +255 22 2125596 | Email:ajirayangu@uwezeshaji.go.tz | Website:www.uwezeshaji.go.tz

ajira.jpg <http://darinsightsmailing.com/link.php?M=17760&N=40&L=34&F=H>

This Post Has One Comment

  1. Rogastian

    Supply details which will be relevant for me daily , update through out for the purpose of getting new comment and news.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *