PROGRAMU YA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI NA MALEZI YA BIASHARA KWA WAHITIMU WA ELIMU YA JUU

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi nchini Tanzania,wameandaa program ya mafunzo ya ujasiriamali na malezi ya biashara kwa vijana waliohitimu mafunzo ya elimu ya juu (Young Graduate Enterprenurship Clinic Program).

Lengo la Programu hii ni kuongeza idadi ya vijana wanawake kwa wanaume katika miradi ya biashara na uzalishaji ili kupunguza tatizo la ajira Nchini.

Mafunzo haya ya ujasiriamali yatajumuisha vijana 50 wenye umri kati ya miaka 18-35, waliomaliza elimu ya juu nchini kwa kipindi cha miaka 5 iliyopita ambao wanataka kuanzisha, kupanua na kuboresha biashara zao.

Mpango huu unaratibiwa na Baraza la Uwezeshaji kwa lengo la kuwezesha vijana kupata ujuzi wa kuanzisha na kuendeleza biashara na kutengeneza nafasi za ajira kwao wenyewe na kwa vijana wengine.

Vijana watakaochaguliwa watapewa mafunzo ya siku nne juu ya mipango ya biashara kabla ya kuendelea na mchujo wa kutafuta washindi watatu wa Young Graduate Entrepreneurship Clinic 2018 ambao watatangazwa na kupatiwa zawadi ya mbegu mtaji.

Mshindi wa kwanza atapewa Milioni 10, mshindi wa pili Milioni 7 huku mshindi wa tatu akipewa Milioni 5.

Washiriki wote watanufaika na msaada wa ushauri wa kitaalamu ili kukuza na kuendeleza biashara zao kwa mwaka mmoja.

Vijana wanakaribishwa kuwasilisha mipango ya rasimu za biashara kwaajili ya mashindano wakitakiwa kujaza fomu ya maombi inayopatikana ndani ya tovuti ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) www.uwezeshaji.go.tz au kupitia barua pepe ya neec@uwezeshaji.go.tz au kufika kwenye ofisi za Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi zilizopo Mtaa wa Kivukoni Front jijini Dar es salaam. Maombi yataanza kupokelewa kuanzia tarehe 21 Agosti 2018 mpaka 11 Septemba 2018.

Baraza linakaribisha vijana wote waliohitimu mafunzo ya elimu ya juu kuchangamkia fursa hii ya uwezeshaji wa maarifa na mitaji.

Pakua “young graduate entrepreneurship clinic form”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *