Sifa za Banda Bora la Kuku

Katika ufugaji kuku kitu kimojawapo cha kuzingatia ni uwepo wa banda bora. Banda bora litawafanya kuku wako wakue vizuri na kuwakinga na magonjwa mbalimbali.

Ujenzi wa banda bora la kuku ni miongoni mwa mambo ya msingi kabisa katika ufugaji bora wa kuku wawe no wa asili au walioboreshwa. Hata hivyo si kila mtindo wa ujenzi unafaa, kwa hiyo ujenzi huo ni lazima uzingatie mahitaji halisi ili ufugaji huo uweze kutoa matokeo bora yanayotarajiwa na mfugaji.

Mambo muhimu katika ujenzi wa banda la kuku ni:

  1. Liingize hewa safi wakati wote
  2. Liwe kavu daima
  3. Liwe na nafasi ya kutosha
  4. Liwe na gharama nafuu lakini la kudumu
  5. Lizuie kuingia wanyama na wadudu hatari kwa kuku
  6. Liwe na nafasi ya kuweka vyombo vya chakula na maji
  7. Lizuie upepo wakati wa baridi kali

Bonyeza hapa kusoma makala yote

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *