Umuhimu wa tafiti kwa wajasiriamali

TAFITI

Tafiti husaidia kuibua changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii ya wajasiriamali

wajasiriamali wengi nchini wanakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa elimu ya kawaida na ile ya biashara, hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kukua kwa biashara zao hivyo kuchangia umaskini kwa wanajamii nchini.
Haya yote yasingejulikana kama kusingekuwa na tafiti mbalimbali ambazo zimekwisha fanyika. Tafiti husaidia sana katika kuibua vitu vilivyojificha vyote vizuri ama vibaya kwa lengo la kuvipatia ufumbuzi wa kisera na kisheria kwa manufaa ya watanzania wote.

MWONGOZO WA UZALISHAJI MAZAO NCHINI

Sekta ya Kilimo ni mhimili wa uchumi wa Tanzania na imekuwa ikichangia Pato la mkulima mmoja mmoja, kaya na Taifa kwa ujumla pia ni tegemeo la mapato ya fedha za ndani na za nje ya nchi. Sekta hii imeajiri zaidi ya asilimia 70 ya idadi ya watu wote nchini na kuzalisha mazao ya chakula na biashara. Mazao makuu ya chakula ya aina ya wanga yanayozalishwa ni pamoja na mahindi, muhogo, mpunga na mtama. Mazao mengine ni ndizi, viazi vitamu na viazi mviringo, ngano, ulezi na uwele. Mazao ya mikunde ni pamoja na maharage, kunde, mbaazi, choroko na njegere. Mazao yote hayo ndiyo yanayochangia Taifa kujitosheleza kwa chakula kwa zaidi ya asilimia 100. Mazao makuu ya biashara ni korosho, miwa kwa ajili ya sukari, pamba, mkonge, tumbaku, pareto, kahawa na chai. Mazao mengine ni ya bustani na mbegu za mafuta.

Pamoja na kujitosheleza kwa chakula na kuchangia katika uchumi wa taifa, takriban mazao yote yamekuwa yakizalishwa kwa tija ndogo kwa maana ya kiasi cha mazao yanayozalishwa kwa eneo. Aidha, uzalishaji umekuwa ukipanda na kushuka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya mazao hayo kuzalishwa katika maeneo yaliyo nje ya ikolojia yake ya asili. Hii imekuwa ni sababu mojawapo kwa baadhi ya maeneo nchini kuwa na tija ndogo na upungufu wa mazao ya chakula na biashara. Uzalishaji wa mazao nje ya ikolojia yake ya asili hupelekea kuwa na tija ndogo na au kuyazalisha kwa gharama kubwa kama vile umwagiliaji maji.

Tanzania inazo Kanda Kuu Saba (7) za Kilimo za Kiikolojia zenye kuwezesha uzalishaji wa mazao ya aina mbalimbali. Kanda hizo ni Kanda ya Kati, Ziwa, Kaskazini, Mashariki, Magharibi, Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kusini. Ili kuzalisha mazao kwa tija na kwa gharama nafuu, Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi imeandaa Mwongozo huu wa uzalishaji mazao unaoainisha mazao ya kipaumbele kwa kila eneo. Mwongozo umeandaliwa ili kuelekeza wawekezaji na wakulima kuchagua zao linaloweza kuzalishwa kwa tija kwa kulingana na hali ya kiikolojia husika. Aidha, mwongozo umezingatia matokeo ya tafiti zilizofanyika nchini kuhusu aina za udongo, hali ya hewa, mtawanyiko wa mvua na aina za mazao yanayofaa kuzalishwa katika kila eneo.

Bonyeza hapa kusoma Mwongozo

 
 
 

TAASISI ZA KIFEDHA NA KUFANIKIWA KWA WAJASIRIAMALI

UTAFITI JUU YA JUKUMU LA TAASISI ZA KIFEDHA KATIKA KUFANIKIWA KWA SHUGHULI ZA KIJASIRIAMALI KWA MKOA WA DAR ES SALAAM.
Imefanywa na:
FRANK GLADSTONE MOSHI

Tafiti hii ililenga kupima jukumu linalofanywa na taasisi za kifedha katika kufanikisha shughuli za wajasiriamali/kijasiriamali. Ingawa wasomi wengi wameoanisha upatikanaji wa huduma za kifedha na kufanikiwa kwa shughuli za kijasiriamali, kwa upande mwingine bado tafiti juu ya jinsi gani taasisi hizi za kifedha zinasaidia kufanikisha shughuli za kijasiriamali hazijafanyika. Utafiti huu ulifanywa katika taasisi kumi za kifedha ambapo ulihusisha: Mabenki ya biashara; taasisi na vikundi vidogo vidogo vya mikopo.

Jumla ya wajasiriamali 95 walichaguliwa kati ya wajasiriamali 93430 wanaopatikana katika mkoa wa Dar es Salaam. Dodoso za aina mbili ziliandaiwa, moja iliandaliwa maalum kwa ajili ya wajasiriamali na nyingine ilikua kwa ajili ya taasisi za kifedha.
Majibu kutoka kwa washiriki yalichakatuliwa kwa kutumia programu maalum ya sayansi ya jamii (S.P.S.S). Tafiti hii iligundua kwamba, taasisi za kifedha zina msaada mdogo katika kufanikisha kwa wajasiriamali. Hii ni kwasababu wajasiriamali wengi hutumia faida wanayoipata au misaada kutoka kwa ndugu na watu wa karibu kama njia ya kujipatia mtaji kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza biashara husika.
Tafiti hii pia ilishauri taasisi za kifedha kufanya matangazo ya kina juu ya huduma zao kwa wale wajasiriamali wasiofahamu na ambao bado hawajaanza kutumia huduma hizo. Ushauri mwingine ulikua kuhusu kupunguza ukali na ugumu wa masharti yaliowekwa kwa ajili ya mikopo, ili wakopaji waweze kukopa kwa riba nafuu. Tafiti hii ilishauri pia, uhitaji wa kufanyika tafiti nyingine ya namna kama hii ila izingatie kuongeza idadi ya washiriki ili kuweza kuboresha majibu kutokana na mitazamo ya watu mbalimbali. (Angalia kiambatanisho cha tafiti hii)

 

Soma ripoti kamili hapa

PANUA MSTAKABALI WAKO KIFEDHA

Na FinScope Tanzania

FinScope Tanzania 2013 ni mzunguko wa tatu wa utafiti wa kutambua na kupima mahitaji na upatikanaji wa huduma za fedha miongoni mwa watu wazima waishio Bara na Zanzibar. Taarifa za utafiti huu zina umuhimu mkubwa kwa maendeleo yahusuyo upatikanaji wa huduma jumuishi za fedha: zinabainisha huduma zinazotumiwa na zisizotumiwa na watu pamoja na sababu zake; vikwazo vya matumizi zaidi ya huduma hizo, na tofauti zinazojibainisha kati ya mkoa na mkoa.

Utafiti huu pia unatoa mwanga kuhusu mitazamo na mienendo ya watu, kuhusu tofauti zao kijinsia, kuhusu maeneo ya mijini na vijijini, mwuelekeo na uwigo wa kuchagua – vyote hivyo vikiwa kwenye mtazamo uliodumu kwa miaka saba sasa.

Utafiti wa kwanza wa FinScope Tanzania ulifanyika mwaka 2006, ukifuatiwa na wa pili mwaka 2009. Watu wazima 8,000 (wenye umri wa zaidi ya miaka 16) walishiriki katika utafiti huu kama sampuli ya kitaifa ya watu wote wazima. Kutokana na aina hii ya utafiti kuwa umefanyika katika nchi nyingi za Afrika, FinScope Tanzania inaweza kutoa ulinganifu mwuafaka kati ya Tanzania na mataifa mengine katika bara hili.

Utafiti huu ni wa muhimu sana kwa taasisi za umma na binafsi kama vile: wizara,

Benki Kuu ya Tanzania, tasnia ya huduma za fedha, kampuni za simu za mkononi, washirika wa maendeleo, vyuo vikuu, asasi za utafiti, asasi zisizo za kiserikali na asasi za kiraia.

Soma ripoti kamili hapa

4. MATATIZO YA VIBALI VYA KUSAFIRISHIA VYAKULA KATIKA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA MASHARIKI

4. MATATIZO YA VIBALI VYA KUSAFIRISHIA VYAKULA KATIKA NCHI ZA UMOJA WA AFRIKA MASHARIKI NA SHIRIKISHO LA MAENDEELO LA KUSINI MWA JANGWA LA SAHARA;

Imefanywa na
Umoja wa safirishaji bidhaa nje ya nchi.

Ripoti hii inawasilisha matokeo ya utafiti uliofanyika juu ya matatizo yanayosababishwa na mahitaji yanayohitajika katika kukamilisha upatikaji wa barua ya ruhusu ya usafirishaji wa chakula kutoka ndani ya Tanzania na kwenda nchi nyingine. Kwa ufupi, tafiti hii iligundua kwamba mchakato huu unasababisha matatizo na usumbufu mkubwa kwa Wasafirishji wa bidhaa hiyo, wafanya biashara wadogowadogo wa mipakani na wakulima wadogo.

Tafiti hii iliweza kugundua kwamba, mahitaji wa kibali hicho cha kusafirisha chakula kinatumika kwa bidhaa za nafaka kama mahindi, mchele, uwele na mtama lakini sio kwa bidhaa za matunda.

Asilimia 61.1 ya wafanyabiashara ya kusafirisha chakula waliohojiwa walisema kuwa wamekwamishwa kwa kiasi na mchakato huu wa vibali; asilimia 19.1 walisema walikwamishwa kwa kiasi kikubwa na mchakato huu, huku asilimia 38.1 nao walikwamishwa kwa kiasi cha kati na mchakato huu. Kwa ujumla, asilimia 56 ambayo ni zaidi ya nusu ya wadau waliohojiwa katika utafiti huu walisema mchakato huu wa vibali umesababisha biashara zao kupata hasara. Hii inaonyesha uhitaji wa haraka wa mchakato wa kuboresha na kupunguza gharama za biashara na mazingira ya usafirishaji wa bidhaa za chakula kwenda Shirikisho la Afrika Mashariki na Sirikisho la maendeleo la nchi za kusini mwa Afrika.

• Ukosekanaji wa uwazi na uelewa juu ya kile kinachohitajika kulinganisha na barua ya kukubalika haviko wazi. Hii inaendelea hadi kuna kipindi barua hutolewa hata kama haihitajiki. “Mfumo wa Uchambuzi wa Uhakika wa Chakula na Lishe” (MUCHALI) inahuusika na kutoa notisi inayohitajika wakati wa kusafirisha nafaka. Tatizo la MUCHALI ni kwamba ukaguzi wake haupo katika ngazi ya wilaya. Kutokana na hili, MUCHALI hutoa notisi ya kila sehemu kuhusu upungufu wa chakula, wakati upungufu huo upo katika sehemu chache tu. Hii husababisha mfuko kuzuia usafirishaji wa chakula hata zile sehemu zilizo na chakula kwa wingi.

• Mchakato wa kupata barua ya kusafirisha bidhaa ni mgumu. Mjasiriamali anaetaka kusafirisha chakula anapitia hatua 5 tofauti ili aweze kupata barua ya ruhusa. Mchakato huu uchukua wiki 2 hadi 4 na unahusisha kusafiri katika wilaya, mikoa na Wizara ya Kilimo and mifugo, na Vyama vya Kulinda Upatikanaji wa vyakula katika mkoa wa Dar es Salaam. Kutokana na hili, biashara ya kusafirisha chakula imewatoa masikini, na kubakia kua biashara ya mawakala wachache wanaojua mchakato mzima wa kupata vibali na barua za ruhusa. Mawakala hawa hutumia vibali hivyo kuwasafirishia watu bidhaa kwa gharama ulani.

• Hamna ushahidi unaoonyesha uwepo wa barua ya ruhusu umepunguza usafirishaji wa mazao ya chakula nje ya nchi hii ni kutokana na uwepo wa rushwa unao ruhusu mazao kupita hata katika kipindi cha zuio.

• Kwa ujumla, barua za ruhusa zimeongeza kuongezeka kwa gharama za kusafirisha bidhaa, muda wa kusubiria, kupoteza kwa mapato/faida na kushuka kwa upinzani kutokana na muda na uhakika wa kusafirisha bidhaa hizo toka ndani ya Tanzania kulinganisha na majirani.

 

Soma ripoti kamili hapa

TOZO ZA KUWEKA NA KUPITISHA MIZIGO KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM

RIPOTI YA UCHAMBUZI WA HALI HALISI YA UTARATIBU WA TOZO ZA KUWEKA NA KUPITISHA MIZIGO KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM
By: Apronius Mbilinyi +255 756 514 644 (apronius2000@yahoo.co.uk)

Bandari ya Dar es Salaam ni bandari kubwa ndani ya Tanzania ambayo inahusika na kutoa na kupokea zaidi ya asilimia 90 ya baishara ya kuuza na kuleta ndani ya nchi; mizigo mingi inayoshughulikiwa ni kwa ajili ya matumizi ya ndani (71%) na 29% iliobaki inapita kuelekea nchi za jirani zisizo na bandari. Bandari ya Dar es Salaam imewekewa miundo mbinu maalum kwa ajili ya kushughulikia mizigo. Miundo mbinu hiyo inasimamia makontena, mizigo kwa ujumla, mafuta, pamoja na magari. Miundo hii ipo ndani ya bandari isipokua sehemu za kupokelea makontena ambazo zinamilikiwa kwa makubaliano baina ya Mamlaka ya bandari na Tanzania International Container Terminal Services (TICS).

Licha ya hivyo, mamlaka ya Bandari ina shughulikia baadhi ya makontena na mizigo mingine kama mafuta na kadhalika. Bandari ina vituo vitano vilivogawanywa kwa makundi mawili; kituo cha mizigo mikubwa ya maji na sehemu ya mizigo mikavu. Vituo hivyo ni: Kituo cha makontena kinachoongozwa na TICS, Kituo cha makontena kinachoongozwa Mamlaka ya bandari, Kitua cha mizigo mizito ya maji, Kituo cha mizigo ya jumla na kituo cha wasafiri.

Bandari pia inahudumia nchi sita ambazo ni Zambia, Malawi, DR Congo, Burundi, Rwanda na Uganda). Bandari ya Dar es Salaam ni mwanzo wa njia mbili kuu za usafirishaji: Njia ya kati inayogudumia na Shirika la reli Tanzania na Njia ya Dar es Salaam inayohudumiwa na reli ya TAZARA. Kwasasa, Bandari ya Dar es Salaam inafanya kazi kama mfanyakazi na mmiliki. Kama mfanyakazi, Bandari inashughulikia kituo kimoja cha makontena na kama mmiliki Bandari imemkodisha Tanzania International Container Services (TICS). Kama mmiliki, Bandari ya Dar es Salaam ina jukulu la kushawishi matumizi, maboresho na maendelezo ya bandari nyingine ndogo za ndani ndani.

Kufuatia mapinduzi ya kiuchumi na ubinafsishaji wa miaka ya 1990, ufanyaji kazi wa Bandari umeboreshwa, na kua moja ya bandari imara katika utoaji wa huduma kwa eneo kubwa ja Afrika chini ya jangwa la Sahara. Mabadiliko haya yalienda sambamba na ongezeko la shughuli za kiuchumi zilizoongeza biashara na uingizajia wa bidhaa ndani ya bandari; hii ilisababisha miundo mbinu ya bandari kushindwa kuhudumia ongezeko hilo kubwa, na hivyo basi ubora wa kazi inayofanywa kuanza kushuka, na kufikia miaka ya 2000, ufanyaji kazi ulikua wa kiwangocha chini sana.

Kudorora kwa huduma katika bandari ya Dar es Salaam kulisababisha kuongezeka kwa muda wa kusubiri mizigo, kuchelewa kwa meli kugeuza, rushwa na gharama za juu za bandari ukilinganisha na bandari nyingine za karibu. Matatizo haya katika bandari yalisababisha kuongeza gharama za ufanyaji biashara ndani ya nchi and kuharibu juhudi za ukuaji wa sekta ya uzalishaji na viwanda kukua kwa ujumla iliofanya Confederation of Tanzania Industries (CTI) kufanya tafiti yua tathmini ya hali halisi ili kuweza kutambua ni jinsi gani gharama za bandari zinakadiriwa kulinganisha na bandari za jirani.

Tafiti hii pia ililenga kukusanya mawazo kutoka kwa watumiaji kwa lengo la kupendekeza njia kwa serikali za jinsi ya kuboresha huduma katika Bandari ya Tanzania.
Taarifa zilitafutwa kutoka kwa wafanyabiashara wa bandari (wauma na binafsi) kama wafanyakazi wa vituo vya bandari; Watoa huduma wa bandari; vyombo vya udhibiti; waingizaji bidhaa; watoaji bidhaa; wasafirishaji; kampuni za kubeba mizigo; na kampuni za kutoa mizigo bandarini. Taarifa nyingine ya ziada ilikusanywa kutoka kwa wadau mbalimbali kutoka bandari ya Mombasa, Kenya na Beira, Msumbiji. Taarifa nyingine zilikusanywa kutoka mitandaoni kama kwenye Tovuti mbalimbali, Taarifa za mwaka za bandari and ripoti nyinginezo.
Matokeo ya Utafiti

 Kuhusu msingi wa kupiga mahesabu ya tozo za bandari; bandari inatumia mfumo maalum wa kiasi cha ununuzi (CIF value) na uzito au ukubwa katika kukadiria mizigoinayofika na kupitishwa bandarini hapo. Wakati mfumo huu wa CIF value unatumika sana katika bandari ya Dar es Salaam, Bandari ya Mombasa inatumia zaidi uzito, ujazo na ukubwa kama kipimo cha kukadiria tozo. Wakati huo bandari ya Beira haina tozo kwa kuweka bidhaa isipokua bidhaa kubwa za maji.

Kitu kingine kilichogundulika katika tafiti hii ni kwamba njia zote mbili za kukadiria katika bandari ya Dar es Salaam zinaongeza gharama hivyo kufanya gharama za kiujumla katika bandari ya Dar es Salaam Kuwa kubwa kuliko zile za bandari ya Mombasa.

Watumiaji wengi wa bandari waliohojiwa hawakuwa na furaha na watoa huduma wa bandari (TPA, TIC, TRA and ICDs etc); mtazamo wao ni kwamba huduma ni za ghali, zikiwa na vikwazo vya kutokuwa bora, rushwa iliokithiri, huduma mbaya kwa wateja na ucheleweshwaji usiokuwa wa lazima. Licha ya hivyo, jitihada za hivi karibuni za waziri kupunguza changamoto zinaleta matumaini ingawaa juhudi hizo binafsi bado hazijawa na uhakika sana.

Uchambuzi wa vipimo vya kawaida unaonyesha kwamba, kwa muda huu, bandari ya Dar es Salaam haifikii malengo ya ndani na ya kimataifa. Hili linaonekana kutokana na bandari kutokua na uwezo wa kufikia malengo yaliowekwa na mamlaka ya usafiri wa ardhini na maji (SUMATRA) kama muda wa kukaa, kwa meli na mizigo kugeuza. Licha ya hivo, mabadiliko ya hivi karibuni yameonyesha jitihada za wazi katika kuboresha ufanyaji kazi wa wizara.

Mapendekezo
Kutokana na uchambuzi wa matokeo ya tafihi hii, tafiti inapendekeza:

Kutokana na ukweli kwamba, njia inayotumia na bandari kutafuta thamani ya tozo ni ya kizamani na inaifanya bandari ya Dar es Salaam kuwa na tozo za juu ukilinganisha na majirani zake, kuna umuhimu wa wadau wa bandari kutoa mapendekezo yao kwa mamlaka husika (SUMATRA) ili mamlaka ya bandari iweze kuwa na njia nyingine mbadala kama zinavotumika na bandari za jirani.

Kuhusiana na huduma za bandari, watu wengi waliohojiwa walisema huduma ni dhaifu na hawajafurahishwa nazo, hivyo watoa huduma wanahitaji kukaa na wadau wa bandari ili waweze kuboresha huduma za bandari kwa ujumla. Bila hivo bandari itapoteza wateja kutoka nchi za jirani kama Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi and DRC.

 

Soma ripoti kamili hapa

MATOKEO YA KIUSHINDANI KUTOKANA NA MABADILIKO YA MAZINGIRA YA BIASHARA

Matokeo ya Kiushindani Kutokana na Mabadilikoya Mazingira ya (CIBER) Udhibiti wa Vikwazo ndani ya sekta ya Utalii Tanzania
Imefanywa na:
Zaki Raheem na Alex Mkindi

Viongozi katika sekta ya utalii Tanzania wanatumia gharama kubwa kwenye biashara kwa upande wa hela na muda. Biashara nyingi zipo tayari kulipa tozo kama tozo zitakua zinajulikana na kupangwa vyema
WAMILIKI WA KAMPUNI ZA UTALII
Kodi na Leseni
• Waongozaji wa shughuli za utalii wanakumbwa na tozo za kodi na leseni 12, ambazo ni wile za cheti cha kusajiliwa, leseni ya biashara, Leseni kutoka kwa Mamlaka ya kutoa leseni kwa wakala wa utalii; Tozo ya ongezeko la thamani; kodi ya ushirika, ushuru wa maendeleo ya ujuzi; huduma za manispaa; Mifuko ya kijamii na vibali vya kazi.

Kanuni za Magari
• Wamilikiwa kampuni za utalii wanakutana na makato, leseni na tozo 11 kwa kila gari watakalo tumia. Hizi zinahusisha Kodi ya ongezeko la thamani; usajili wa magari na ukaguzi; leseni ya barabara; Bima, nembo ya ulinzi wa moto; nembo ya usalma, and nembo kutoka Mamlaka ya usafiri wa ardhini na kwenye maji (SUMATRA)
• Inalazimisha wamiliki wageni wa kampuni za utalii kulipia magari 5 hadi 10 inaaminika kama ni kikwazo cha watu kushiriki
• Ushuru wa kuingiza bidhaa na kodi ya ongezeko la thamani inaongeza hadi asilimia 62 ya gharama halisi ya gari.
• Ukosekanaji wa mikopo kwa wajasiriamali unaongeza pia mzigo kwa watu hao. Huku wamiliki kutoka nje ya nchi wanaweza kupata mikopo nafuu kutoka benki za kwao, benki za Kitanzania hazina mikopo maalum kwa ajili ya shughuli za utalii.
Tozo
• Tanzania ina tozo za juu zakuingia bungani kuliko nchi yoyote ya eneo la Kusini na Mashariki mwa bara la Afrika.
• Tozo zisizosimamiwa kwenye barabara za kitaifa zinazuia uwezo wa mmiliki wa kampuni za utalii kupangilia safari za utalii.
• Ukosekanaji wa mfumo wa malipo kabla ya matumizi unaleta mzigo kwa uongozi, na hofu za kiusalama kwa wamiliki wa kampuni za utalii.

Wamiliki wa Hoteli
• Waongozaji wa shughuli za utalii wanakumbwa na tozo za kodi na leseni si chini ya 10, ambazo zinahusisha tozo za makampuni; kodi ya mgao wa zuio; ushuru wa mishahara; Kodi ya mali; ushuru wa huduma za manispaa; kodi ya ardhi; vibali vya kazi, Makato ya Mamlaka ya Usalama na Afya kazini; Ushuru wa COSOTA; Vibali vya mamlaka ya dawa na chakula na tozo za mabango.
• Safari pia za bila taarifa za viongozi mbalimbali wa serikali zinaendelea kua mzigo kwa wamiliki wa hoteli
• Ubadilikaji wa mara kwa mara wa kodi, tozo na malipo mbalimbali unaharibu mpangilio wa jumla wa wamiliki wa hoteli
• Mashine za kielekitroniki zinaboresha na kutoa fursa za kuongeza mapato ya kijumla yanayotokana na kodi, shida inakuja upande wa malipo yale yanayohusisha fedha za kigeni.

MAPENDEKEO
• Kupunguza mizigo ya kiungozi
• Kupunguza nyaraka zinazohitajika
• Kupunguza toza za kusajiri magari
• Tozo za manispaa ziunganishwe na tozo za mabango
(Angalia kiambatanishi)

 

Soma ripoti kamili hapa

KUBORESHAMCHANGO WA WAJASIRIAMALI WADOGO KATIKA KUTOA AJIRA NA KUPUNGUZA UMASIKINI

SHIRIKISHO LA WAAJIRI TANZANIA – KUBORESHAMCHANGO WA WAJASIRIAMALI WADOGO KATIKA KUTOA AJIRA NA KUPUNGUZA UMASIKINI NDANI YA MKAKATI WA KITAIFA WA KUPUNGUZA UMASKINI.

Na: Dr. Donath R. Olomiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kitengo cha Ujasiriamali (UDEC)

Shirikisho la Waajiri Tanzania umefanya uamuzi wa kimchakato wa kuchukua jukumu la ukaribu zaidi kwa uendeleaji wa shughuli za kijasiriamali, kama njia kutimiza lengo la kuboresha mahusiano ya wafanakazi katika sekta binafsi. Katika mwaka 2004/5 shirikisho lilifanya tafiti katika msukumo wa sera, sheria na kanuni mkazo ukiwa umewekwa kwenye upatikanaji wa masoko. Tafiti hii ilifanyika chini ya msaada kutoka Shirika la Kimataifa la Kazi, chini ya mradi uliotengenezwa maalum kwa ajili ya kuboresha mchango wa Wajasiriamali katika kuboresha mchango wa wajasiriamali katika kutoa ajira na kupunguza umasikini ndani ya mchakato wa kitaifa wa kupunguza umasikini.

Tafiti hii iligundua kwamba, sharia ya manunuzi ya uma na viwango na kanuni zake ni moja ya kikwazo kikubwa kinachozuia upatikanaji wa masoko kwa wajasiriamali. Hii ilisababisha pia tafiti ya kina ifanyike kwenye mambo hayo mawili. Baadae wahusika waliamua kutoa matokeo ya utafiti na wadau wengine kwaajili ya kuipitisha na pia kama ajenda ya kuwa husisha katika mchakato wa mabadiliko. Nyaraka hii inawasilisha matokeo ya utafiti huu pamoja na michango iliopatikana kutokana na mkutano na wadau wengine.

NJIA YA UTAFITI
Tafiti hii iifanyika kwa nyia ya kupitia machapisho mbalimbali. Nyanja nne zilizotathiminiwa kuwa na umuhimu kwenye upatikanaji wa masoko kwa wajasiriamali zilichagulia. Nyanja hizo ni: Upatikanaji fedha, Kodi, Viwango na Biashara kwa ujumla. Matoke kwa ujumla yalionyesha eneo lenye mchango mkubwa katika kiwango cha mafanikio cha wajasiriamali ni lile lenye uhusiano na manunuzi ya serikali na viwango vya chakula. Uchambuzi wa kina ulifanyika kwa njia ya mahojiano na maafisa wa ngazi ya juu katika vyombo husika.

Mambo mbalimbali na vikwazo vinavohusiana na manunuzi ya uma
kuna fursa nyinyi kwa wajasiriamali katika kuuza bidhaa kwenye taasis za serikali kuu na serikali za mitaa. Ufikiaji wa masoko haya unakwamishwa kwa kiwango kikubwa kwenye zile sekta ambazo kuna makampuni mengine ya kigeni. Mabadiliko ya hivi karibuni katika sheria ya manunuziya uma (2004) na kanuni husika, yaliyosababisha uanzishwaji wa Mamlaka ya kudhibiti manunuzi ya uma, Mamlaka ya kushughulikia malalamiko ya manunuzi ya uma na kutoa upendeleo kwa wafanyabiashara wa ndani ambao kwa kiasi kikubwa wengi ni wajasiriamali. Upendeleo huo unaweza kuhusisha: upendeleo wa kipekee kwa kampuni za wazawa kwa ajili ya miradi ya hadi 50 milioni had 1 bilioni (kutegemeana na aina ya kazi); upendeleo wa makampuni yanayomilikiwa na wazawa kuanzia 4% hadi 10% (kutegemeana na uhusikaji wa wazawa); upendeleo kwa bidhaa zinazozalishwa ndani au zilizochimbwa ndani kwa hadi 15% na kugawanywa kwa mikataba ili kuifanya iweze kupatikana kwa makampuni ya ndani.

Licha ya juhudi hizi, wajasiriamali wanaweza wasifaidike kutokana na maendeleo haya. Hadi sasa kanuni na miongozo ya sheria ya manunuzi ya uma, bado haijafahamika vizuri kwa watu wote. Sheria hii inaamini kwamba manunuzi ya serikali yatakua kwa wale wajasiriamali waliojiimarisha vizuri zaidi. Kwasababu hii, mawasiliano mengi hufanyika kwa lugha ya kiingereza, pia kwa njia ya mitandao na magazeti mengine ambayo hufikia sehemu ndogo sana ya wajasiriamali. Matokeo yake uelewa wa nafasi za mafanikio katika serikali kuu na za mitaa, mashirika ya uma na washiriki wa biashara unakua mdogo.
Vizuizi vinavohusiana naviwangovya chakula

Sheria kuu zinazosimamaia chakula na madawa Tanzania ni Sheria ya Chakula, madawa na vipodozi ya mwaka 2001 na Sheria ya Viwango ya mwaka 1975 na kufanyiwa marekebisho 1977. Kitu kikubwa cha viwango kinachoathiri wajasiriamali katika kufikia masoko ni (i) Sheria na kanuni ziko mbali sana kufikiwa na wajasiriamali hawa (ii) Kutokueleweka vizuri kwa umuhimu wa baadhi ya mamlaka kama shirika la viwango Tanzania (iii) Mapungufu kwenye uongozi wa sharia hizo mbili. Kua na nembo ya ubora ni hiari. Kuna sintofahamu kubwa juu ya viwango na mahitaji

Kazi za shirika la viwango hazifahamiki vizuri na wananchi wa kawaida. Walaji, wauzaji wa rejareja, mashirika na wajasiriamali wanaamini mtu hawezi uza bidhaa yoyote bila kua na ruhusa na uthibitisho wa shirika hilo. Hili linatokana na mawasiliano yasiokidhi haja baina ya TBS na TFDA. Nyaraka nyingi zipo Dar es Salaam na zimeandikwa kwa Kiingereza, hii inamaanisha watu wasioweza kusoma na kuandika kiingereza na wale walio nje ya Dar es Salaam hawawezi pata nyaraka hizi. Maktaba zao hazina nyaraka rahisi za kusoma kuhusu uelewa wa utaratibu na mwongozo inayoweza kua ya muhimu kwa wajasiriamali.
Ingawa TBS na TFDA wanatoa huduma za msingi sana kwa wajasiriamali, wao wana ofisi Dar es Salaam tu. Hii husababisha gharama kwa wajasiriamali za kutuma na bidhaa zije kufanyiwa uchunguzi Dar es Salaam.

Hitimisho na Mapendekezo

Imependekezwa sharia ya manunuzi kupitisha msimamo mpana zaidi katika kuongeza ufikwaji wa manunuzi ya uma, kwa kuruhusu wajasiriamali wa aina mbalimbali waweze pata mikataba ya manunuzi ya uma. Nyaraka kutoka Bodi ya Manunuzi ya Umma, TBS na TFDA zitengenezwe kwa namna itakayowawezesha watu mbalimbali kuzisoma. Miongozo itengenezwe ka ajili ya serikari za mitaa na wajsiriamali. Wizara husika, iwape wafanyakazi wake maelezo juu ya aina, uhalisia, na umuhimu wa wajsiriamali, pia kuzifanyia mapitio sheria na kanuni ziweze kufanana na ufuatiliajina uwezo wa kukidhi mahitaji. Wizara pia irahisishe na kuvigawanya vitengo vya upimaji katika sehemu mbalimbali za nchi.

Vyama vya wafanyabiashara navyo vijitahidi kutafuta na kusambaza taarifa juu ya viwangona mahitaji ya manunuzi ya uma. Vyama hivi vifanye kazi na mamlaka husika ili kuweza kutengeneza njia sahihi ya kuwasiliana. Pia waweze kugundua vikwazo vya kiuwezo nakuja na mipango ya kuvishughulikia.
Nini kifuatwe

Wakati wa mkutano na wadau, washiriki walikubalina kuwa ripoti hii inafanana na hali halisi ya manunuzi na vikwazo vilivoorodheshwa ni sahii. Mapendekezo yaliotolewa pia yalionekana ni njia sahihi wakutatua vipingamizi vilivyopo. Kama kuamua nini kifwate, waliamua

• Ripoti hii isambazwe kwa wadau mbalimbali wanaotakiwa kufanyia kazi mawazo haya. Hii ijumuishe, mamlaka za udhibiti, vyama vya wafanyabiashara, Wizara ya fedha, Wizara ya Afya na kadhalika.

• Kundi la wafanyakazi liwe na wawakilishi kutoka vyama vya muhimu vya wafanya biashara na malaka za udhibiti waje na njia na namna ya kuboresha usambazaji wa taarifa

• Biashara chache zichaguliwe na kusaidiwa kwa kupewa uelewa na uwezo wa kuweza kufikia viwango vya TFDA na TBS. Baadae biashara hizi zitumiwe kama mfano kwa wafanyabiashara wengine juu ya njia na mbinu za kufwata katika kuweza kupata vibali vyote husika

 

Read full report here