Usindikaji wa chakula

Usindikaji wa chakula ni kile kitendo cha kubadili bidhaa ghafi za kilimo kiumbo na kikemikali na kuwa chakula tayari. Katika utayarishaji, usindikaji wa chakula unahusisha kuchanganya viungo ghafi vya chakula ili kuweza kupata chakula ambacho kiko tayari kutumiwa na wahitaji. Kama ilivyo katika nchi nyingine, wajasiriamali ndani ya Tanzania wanaweza kujihusisha na biashara ya kusindika chakula.

Vitu vya kuzingatia wakati wa kuanzisha biashara ya chakula

• Eneo la biashara
Mtu anapotaka kuanzisha biashara ya kusindika chakula, eneo huwa ni jambo la msingi la kuzingatia. Kwa kiasi kikubwa, eneo huwa linachaguliwa kwa kuzingatia ukaribu wa soko na ukaribu wa upatikanaji wa mali ghafi za uzalishaji. Ili kupunguza gharama zinazoweza kuongezeka wakati wa uzalishaji, ni vizuri biashara ianzishwe karibu na soko au sehemu ambapo mali ghafi zinapatikana.

• Wazo la bidhaa
Kwenye hili, ni lazima mtu awe na wazo la bidhaa analotaka kuleta kwenye biashara. Kama mjasiriamali ni lazima ujiulize maswali kadhaa ya msingi unayotaka kuyaendeleza na kuwa biashara au bidhaa. Maswali haya yanaweza kuhusisha

i. Nini bidhaa yako?
ii. Nani ni wateja wako?
iii. Je una wapinzani?

• Usalama wa chakula (Sheria na kanuni zinazosimamia usindikaji wa chakula)
Kama msindikaji wa chakula, usalama wa chakula ni lazima uwe kipaumbile chako namba moja. Ili kuzuia matatizo yanayoweza kutokea kutokana na usalama mbovu wa chakula ni lazima kuwa na kituo kilichojengwa vizuri kwa ajili ya usindikaji, pia unatakiwa uweke taratibu za kuzuia uchafuzi wa bidhaa, njia sahihi ya kulinda usafi wa chakula, na mfumo sahihi wa kuzui ukuaji na mazalia ya wadudu. Kifungu cha 28 cha sheria ya Chakula, dawa na vipodozi ya mwaka 2003 kinakataza kutengeneza, kuuza , kusambaza, au kuingiza chakula chochote isipokua kwa vile vyakula ambavyo vimesajiliwa na mamlaka ya chakula, dawa na vipodozi (TFDA). (Angalia ambatanisho la sheria husika).

Ufungaji na Uwekaji wa alama

Ufungaji ni kile kitendo cha kuweka bidhaa katika kifungio sahihi. Ufungaji ni kitu cha muhimu kwa sababu hulinda bidhaa yako dhidi ya uharibifu au uchafuzi usiotarajiwa. Pia ufungaji huweza kuwa kama njia ya kutangaza biashara, kwani umbo zuri la ufungaji huweza kumvutia mtumiaji wa bidhaa husika.
Kuweka alama (labeling) kwa upande mwingine, ni kile kitendo cha kuweka kipande cha karatasi, nguo, chuma, au vifaa vingine juu ya kifungio cha bidhaa. Mahitaji ya kuweka alama kwenye kifungio hutofautiana kati ya bidhaa na bidhaa, ila kwa kawaida alama huhusisha vitu kama utambulisho wa bidhaa, uzito au ujazo, taarifa za mzalishaji, tarehe ya mwisho wa matumizi, maelekezo ya uhifadhi na taarifa za lishe.
Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi imetoa angalizo na maelekezo ya vitu vya msingi vya kuwepo ndani ya alama, vitu hivyo ni:

i. Jina la bidhaa
ii. Orodha ya viungo
iii. Aina ya bidhaa (Mf. Mboga mboga, nyama)
iv. Jina na Anwani ya mtengenezaji
v. Nchi zinapotokea
vi. Kundi la utambulisho
vii. Maelekezo ya uhifadhi
viii. Malekezo ya matumizi

• Bima

Bima ni mabadilishano kama fidia kati ya mmiliki wa biashara na kampuni ya bima katika kiwango maalumu kwa muhula/kipindi maalumu. Lengo kuu la biashara ya bima ni kudhibiti au kuondokana na hatari ambayo sio ya lazima. Aina za bima zilizopo zinahusisha bima ya maisha na bima ya mali. Wakati wa kutafuta bima mjasiriamali awasiliane na wazalishaji wengine au marafiki kwa ajili ya taarifa ya watoaji wa bima.
Matatizo yanayowakumba wajasiriamali wengi wa kusindika chakula

• Kutokuwa na elimu sahihi ya viwango, mahitaji, vituo vya kufunga vitu, sheria za na kanuni vyakula
• Viwango vya mali ghafi
• Taarifa zisizo sahii juu ya bei na viwango
• Ukosefu wa miundo mbinu juu ya vitengo vya tafiti na kujaribu vitu
Mahitaji ya Kupata kibali cha kusindika chakula

ENEO LA BIASHARA
i. Eneo la chakula au kutengenezea chakula ni lazima liwe mbali na vyanzo vya uchafu wa aina mbali mbalia kama harufu, moshi, au sehemu ya mazalia ya wadudu
ii. Anuani kamili ya kitalu na ya posta lazima iandikwe kwenye fomu ya maombi ili iweze kurahisisha usimamizi na ukaguzi

UJENGAJI WA ENEO LA BIASHARA

i. Eneo la biashara lijengwe kwa ajili ya mahitaji ya biashara tu, na lisihusishwe na biashara yoyote inayoweza kusababisha kuhatarisha usalama wa chakula
ii. Jengo lijengwe kwa namna itakayorahisisha ufanyaji usafi na matengenezo pale yatakapo hitajika
iii. Jengo la kutengenezea chakula lazima liwe na

a) Eneo la kutosha la kuhifadhi na kuweka vifaa vya kufanyia usafi
b) Eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya zile shughuli zinazoweza kuhatarisha usalama wa chakula
c) Liwe linaruhusu mwanga wa kutosha ili kurahisisha ufanyaji kazi
d) Kuwe na ulinzi wa kutosha dhidi ya wanyama waharibifu kama panya, ndege n.k.
e) Sakafu, kuta na paa za jengo ziwe zinaweza kusafishika na zihakikishwe zipo salama kila wakati.
f) Utengenezaji wa kona au sehemu zinazovuja ni lazima ufanyike kwa wakati kuepusha kuhatarisha usalama wa chakula
g) Eneo la kufanyia kazi kati ya mashine na ukuta liwe kubwa ili kuepusha uwezekano wa mfanyakazi kuhatarisha usalama wa chakula

MASHINE, VIFAA NA MAENEO YA KUWEKEA CHAKULA
i. Kila kifaa au mashine zinazotumika kwa ajili ya matengenezo ya chakula ziwe ni maalum na zinafaa kwa matumizi hayo. Ziwe zimetengenezwa vizuri na zinasafishika
ii. Sehemu yoyote ambapo chakula kinawekwa lazima pawe pasafi, hapana mashimo, na pawe panaweza kufanyiwa usafi mara kwa mara bira kuharibika
iii. Vifaa vinavyotumika kuwekea au kukatia chakula view vingi, ili kutoa muda wa kuweza kusafishwa vizuri kabla havijatumiwa tena.

WATU/WAHUSIKA
i. Wamiliki wa eneo la chakula lazima wahakikishe mtu anae umwa magonjwa ya kuambukiza haruhusiwi kushika vyakula au zile sehemu za kuwekea chakula
ii. Ukaguzi wa kina wa kiafya kwa wafanyakazi ufanyike kabla ya kuajiliwa na kila baada ya miezi sita
iii. Wafanyakazi lazima wawe na ufundi kutoka vyuo vya mafunzo vinavyotambulika
iv. Taarifa za ukaguzi wa afya wa wafanyakazi ziwekwe sehemu maalum na ziwe zinaweza kupatika kirahisi kwa ajili ya ukaguzi

SEHEMU YA KUHIFADHIA VITU
i. Eneo la kutengenezea chakula lazima lilindwe, ili lisiathiriwe na uharibifu na ni lazima lifanyiwe matengenezo na ukarabati mara kwa mara
ii. Vifaa vya kuhakikisha mazingiza ya uhifadhi uko sawa kama viyoyozi na majokofu ni lazima yawepo nay awe katika hali joto inayostahili
iii. Vyakula vyote viwekwe mbali na sakafi ila katika makabati maalum ya kuwekea vyakula hivyo
iv. Sehemu ya kuhifadhia vyakula vya nafaka, lazima vichunguzwe kwa ajili ya kuangalia hali joto na wadudu waharibifu na taarifa ziwekwe vizuri katika sehemu husika.

USAFI
i. Majengo yote yanayohusika na chakula lazima yawe yana mindombinu inayoruhusu usafi kufanyika kirahisi
ii. Lazima kuwe na maji ya kutosha ya moto na baridi kwa ajili ya matumizi husika
iii. Lazima kuwe na miundombinu sahii ya utupaji taka
iv. Lazima kuwe na vifaa vya ulinzi na vya kuhakikisha usafi kwa ajili ya wafanyakazi
v. Watu wanaoshika vyakula lazima wawe wasafi na wajiepusha na tabia zinazoweza hatarisha usalama wa chakula kama uvutaji wa sigara, kupiga chafya na kukohoa mbele ya chakula, kuchokonoa pua na kulamba vidole
vi. Lazima kuwe na vifaa vya kutosha kwa ajili ya kunawa mikono, kama maji, sabuni na vifaa vya kusafishia kucha ili kuepusha kuchafua mikono kunakoweza kuharibu usafi wa chakula
vii. Milango itengenezwe ka jinsi ya kufunguka upande wote, ili kuepusha kuchafua chakula

NYARAKA NA UHIFADHI WAKE
Mtu yoyote anayemiliki biashara ya chakula lazima ahakikishe nyaraka zifuatazo zinahifadhiwa
i. Kibali cha kuingiza au nyaraka za manunuzi
ii. Nyaraka za usafi
iii. Kitabu cha kumbukumbu au mfumo maalum wa kuhifadhi taarifa
iv. Kitabu cha wageni
v. Stakabadhi za mauzo (kwa wauzaji wa jumla)
vi. Kitabu cha taarifa za ukaguzi
vii. Taarifa za ukaguzi wa kiafya (Pale zinapohitajika)
viii. Orodha kwa ajili ya vyakula vilivyokataliwa, haribika au tolewa kwenye orodha ya bidhaa
ix. Kitabu cha kusimamia malalamiko
x. Kanunu ya 2011 ya Tanzania kuhusu usafi wa vyakula, dawa na vipodozi
xi. Kanuni ya 2011 ya Tanzania kuhusu malipo na tozo kwenye biashara ya vyakula, dawa na vipodozi

KURUDIWA KWA MAOMBI, KUKATALIWA NA KUONDOLEWA
i. Mwombaji anatakiwa awe na uwezo wa kuzitafta na kurudihsa bidhaa zote zilizoenakana zina madhara au zilizozuiwa
ii. Kwa ile nia ya kutoa bidhaa sokoni ilioamliwa na miuuzaji, mamlaka (TFDA) itapewa taarifa na lengo/sababu ya kuzitoa bidhaa hizo
iii. Zoezi la kurudisha bidhaa liwe linauwezo wa kuwafikia hadi wale wauzajia wa rejareja
iv. Taarifa za usambazaji ziwekwe tayari kwa ajili ya mtu anaeongoza zoezi hilo na ihakikishe ina taarifa za kutosha kuhusu bidhaa hiyo.
v. Utupaji au uchomaji wz bidhaa zilizotolewa sokoni ufanyike ndani ya mwezi mmoja baada ya zoezi la kutoa bidhaa sokoni kukamilika. Zoezi hili lifanyike chini ya msimamizi kutoka kwenye mamlaka husika (TFDA), au mkaguzi kutoka taasisi nyingine za serikali.