Wanaofanya biashara kienyeji wapewa mda kurasimisha

Wakala wa Usajili wa biashara na leseni (Brela) wametoa mda wa miezi miwili kwa wafanyabiashara wanaotumia majina ya biashara pasipo kusajiliwa wafanye hivyo haraka.

Ofisa mtendaji mkuu wa Brela Frank Kanyusi alisema hayo katika zoezi la kutoa elimu na kurasimisha majina ya biashara na kampuni linaloendelea katika mikoa mbalimbali. Imebainika kuwa wafanyabiashara wengi wanatumia majina ya biashara pasipo kuyasajili.

“Sheria ya majina ya biashara inamtaka mfanyabiashara kusajili jina la biashara yake ndani ya siku 28 kutoka aanze kulitumia, kinyume na hapo atakuwa amevunja sheria ya majina ya biashara,” alisema Kanyusi.

Alisema kuwa baada ya mda huo kupita patakuwa na msako nchi nzima ili kuwabaini wale wote wanaotumia majina ya biashara pasipo kusajiri na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria au kuwatoza faini.

Kwa sasa usajili wa majina ya biashara umerahisishwa kwani unafanywa kwa njia ya mtandao kwa kutembelea tovuti ya wakala ili kupata maelezo yote ya namna ya kusajili jina la biashara.

“Kwa kurasimisha biashara serikali itapata mapato kwani wigo wa walipa kodi utaongezeka na pia itakuwa faida kwa wafanyabiashara katika kujengewa mazingira bora ya kufanya biashara.

Rasimisha jina la biashara yako kwa kubonyeza hapa

Chanzo: Majira tar 10

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *